Ticker

6/recent/ticker-posts

TGNP YAZITAKA ASASI ZA KIRAIA KUUNGANISHA NGUVU KWA PAMOJA KUPIGANIA MASUALA YENYE MLENGO WA JINSIA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imezitaka Asasi za Kiraia kuhakikisha yanashiriki kikamilifu katika malengo yao katika suala la maendeleo endelevu yenye mlengo wa kijinsia kwa maslahi mapana ya Taifa,bila kuacha kundi lolote.

Hayo yamesemwa leo Desemba 21,2023 Jijini Dar es Salaam na Afisa Programu na Sera kutoka Idara ya Ujenzi wa harakati nguvu za pamoja (TGNP) Bi.Logathe Loakaki alipokuwa akizungumza katika warsha ya Asasi za kiraia ambayo imehusisha washiriki kutoka Kanda mbalimbali nchini.

Aidha amesema kuwa wanatamani kuona mashirika mbalimbali yakijitoa kwa hiari kwa ajili ya kuboresha mchakato huo wa usawa wa kijinsia katika suala la maendeleo endelevu.

Ameeleza kuwa Asasi za kiraia wamehudhuria kwa ajili ya kujadili kuhusiana na Mchakato wa ufatiliaji wa suala la maendeleo endelevu wa hiari ambalo limejikita katika usawa wa kijinsia

Bi.Logathe amesema kuwa katika mchakato wa ufutialiaji wa hiari walianza tangu hapo mwaka jana na alieleza kuwa mchakato huo huwa unafanyika kila baada ya miaka minne na kwa mara ya mwisho ulikuwa 2019 ambapo mwaka jana waliweza kukutana kwa pamoja na kukubaliana jinsi wanavyoweza kuchagiza katika ufutialiaji huo katika suala la maendeleo endelevu.

"Tulifanya mchakato huo na baadae tulikutana watu wachache na kuendelea kujadiri kwa kina na kuchagiza katika ripoti ile na ilikua ni safari ya takribani miezi 10 na hatimae mwezi wa tisa tulifanikiwa kuzindua ripoti ya pamoja ijulikanayo kama voluntary national report (VNR)" Bi.Lyayakaki Amesema.

Pamoja na hayo amesema kuwa wameangazia suala la dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050 wakati wa Kuelekea mwisho wa dira ya Taifa 2025 kujua mapungufu ni yapi na mafanikio ni yapi ili kwenda na mapendekezo kwa serikali ili dira itakayo andaliwa iwe ni dira ya watu wote kwani ni dira ya miaka 25 iwe ni dira yenye mlengo wa kijinsia isiyo acha baadi yabmakundi nyuma.

Kwa upande wake,Mwana harakati wa Jinsia kutoka Taasisi ya Yowed Foundation Bw.Mophat Mapunda , amesema kuwa wamejadiri kuhusiana na dira ya Taifa na kutambua kuwa kulikuwa kuna zaidi ya malengo matano na bado zilikua hazijajikita katika mlengo wa kijinsia.

"Kwahiyo tunajaribu kuangalia sehemu gani kuna nafasi zilizo achwa wazi maana tunajua tunaenda mwisho wa bajeti kwa maana tunaangalia masula mbalimbali pamoja na suala la bajeti Kama wadau tunaenda kuangalia ni jinsi gani tunaweza kufanya uchechemuzi kwa ajili ya kuziba nafasi". Ameeleza.

Naye Meneja wa Programu kutoka Shirika la Builders of Future Africa,Bw.Frank Sakalani ameeleza kuwa Asasi za kiraia zimekutana kujadiri mambo ambayo hayakuwepo katika mpango wa maendeleo endelevu uliopita na kuyatambua ili kuyaweka katika dira mpya ya 2050 ili ioneshe wazi katika mambo ya masuala ya kijinsia.

Post a Comment

0 Comments