Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI KIJAJI - TUNAKILA SABABU YA KUWALINDA WAWEKEZAJI WENYE VIWANDA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dk.Ashatu Kijaji amewaomba vijana wa kitanzania kuwa na uadilifu na kujituma wanapopata hizo ajira waweke kipaombele kwenye uadilifu wao wafanyakazi zile ambazo wameaminiwa kufanya ili waendelee kunufaika kwa pamoja na kuimarisha uchumi wa mmoja mmoja na Taifa letu kwa ujumla.

Hayo amebainisha leo Disemba 21 jijini Dar es Salaam na Waziri huyo baada ya kutembelea kiwanda cha Chemicotex kilichopo Mbezi Beach Jogoo amesema wanakila sababu ya kuwalinda wawekezaji wenye viwanda wanawapa ajira ili waendelee kunufaika kwa pamoja.

Amesema ametembelea kiwanda hicho kuona bidhaa wanazozalisha na pili wameongea na wafanyakazi kusikiliza hali yao wanachukulia je mazingira yao ya kazi na kuna viwanda mbalimbali ndani ya eneo hilo la hekari 17 hapa jiji.

"Nimpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa sababu ametengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na ufanyaji biashara tunaona wawekezaji wanafuraha na amani wamekuja kuwekeza na wanaendelea kuzalisha,"amesema Dk. Kijaji.

Amesema huyo ni mtanzania ameajiri watanzania 1000 hawa ni moja kwa moja wanafanyakazi kiwandani na wanaajiri 1000 na zaidi ya 1000 wanauza kule nje bidhaa zinauzwa ni za kiwanda hicho na vijana wakiwa na amani na furaha.

"Ukiacha hawa 1000 tulipoanzia kwenye kiwanda kinazalisha dawa za meno whitdent ambayo hii ni ya hapa hapa nyumbani inatengenezwa nyumbani popote ukiona na bidhaa ya kutoka nyumbani imetengenezwa na watanzania wenzetu walioajiriwa kwenye kiwanda hiki,"amesema.

Amesema kwa sababu kila unapokwenda unakutana na bidhaa za kiwanda hicho ni muhimu sana kutambua hilo na unazalisha unatengeneza ajira kwa vijana na wanapata faida na waendelee kuwekeza na mitaji yao ipo salama.

Ameeleza kuwa kilichompa faraja zaidi ya asilimia 60 ya wafanyakazi hawa 1000 ni wanawake hivyo inaeleza mahili hapa ni salama na wote niliongea na wanashukuru wanalelewa vizuri.

Dk. Kijaji mesema kama kungekuwa na mazingira magumu ya kazi wangekuja na kuondoka wengi wanafurahia ajira yao na wanaridhika na mishahara yao.

"Wapo kwenye dunia ya kupambana na kushindana sisi tupo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki mmesikia bidhaa inayotengeneza hapa inauzwa kwenye nchi sita ndani ya Afrika na duniani tunapeleka bidhaa zetu,"ameongeza.

Aidha amesema wanaendelea kuimarisha Tanzania ya viwanda wanapotekeleza dira ya Taifa wanakwenda kuhitimisha mwaka 2025 na imesisitiza viwanda kwani ndo sehemu pekee watanzania wengi wanapata ajira zao.

Ameeleza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo wanakwenda kuhitimisha ya mwaka 2025 walianza kutekeleza mwaka 2000 ilitoa mwanga mkubwa kwa wenye viwanda kuendelea kuja Tanzania na kuwekeza pamoja nasi.

Amesema wanavyojua dunia ya sasa ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda hata dira inayoandaliwa sasa itawapa nafasi kubwa wenye viwanda kwa sababu sehemu pekee inawapa ajira watanzania ukiachana na kilimo na sekta ya viwanda kutoa mchango miaka 25 na miaka 50 ijayo

Dk. Kijaji ametoa wito wake kwa wamiliki wa viwanda ni kuendelea kufurahia mazingira bora ya ufanyaji biashara ndani ya Taifa letu na mazingira bora ya uwekezaji kwani Rais Dk.Samia amefanya vizuri wote wana amani.

Naye Mwenyekiti wa Kiwanda cha Chemicotex, Yogesh Manek amesema leo wamepata bahati ya kutembelewa na Waziri Dk.Kijaji na kuona bidhaa wanazozalisha.

Amesema katika kiwanda hicho wanazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo dawa za meno whitdent vipodozi, Kream na zinginezo.

"Asilimia kubwa ya watanzania wanatumia bidhaa ya kiwanda hiki tumeajiri jumla ya watu 1000 kati ya hao 550 wanawake na 450 wanaume na walemavu 6 hii ni fursa kwa.mtu yeyote anataka kufanya kazi,"amesema Manek.

Aidha amesema hali ya biashara kwa sasa ni nzuri kwa sababu wanafursa ya kufanya kazi na wanapeleka bidhaa zao nchi sita ikiwemo Rwanda, Unganda Uganda, Kenya, Burundi na Congo pamoja na soko la Tanzania.

Ameongeza kuwa mazingira ya biashara kwa sasa ni mazuri na mazingira ya wafanyakazi mazuri.

Post a Comment

0 Comments