Ticker

6/recent/ticker-posts

ADAKWA NA POLISI AKITAKA KUTAPELI SH M. 1.5


Na Hamida Kamchalla, TANGA.
 
JESHI la Polisi Mkoani Tanga, linamshikilia Ramadhani Mbano (21) akituhumiwa kwa kosa la kumteka mtoto mwenye miaka mitatu na miezi nane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema, katika tukio hilo polisi inamsikilia Ramadhani Adinani Mbano aliyekutwa akiwa na Mtoto aliyetekwa.


Kamanda Mchunguzi amesema, mtoto huyo alikuwa akiishi eneo la Mji Mpya wilayani Korogwe na alitekwa akiwa anatoka nyumba ya jirani kucheza.


"Baada ya Polisi kupata taarifa msako mkali na uchunguzi ulianza kumfuatilia mtoto huyo"alisema Kamanda Mchunguzi.


Aidha Kamanda huyo alisema,baadaye mzazi aliyetoa taarifa polisi juu ya kupotelewa na mtoto wake alipokea simu kutoka kwa mtu asiyefahamika ikimtaka kutoa Shilingi 1.5 Mil ili kumwachia Mtoto.


"Baadaye Mzazi alipigiwa simu na mtu asiyefahamika ikimtaka kutoa sh milioni 1.5 ili kumwachia mtoto na asipompatia hizo fedha angemdhuru mtoto huyo" amesema Kamanda Mchunguzi.


Aliendelea kusema kuwa, uchunguzi na msako vilianza tarehe Januari 25 mwaka huu, majira ya mchana, na mtoto alipatikana kitongoji cha Sagama 'A', kijiji cha Kwamkono, kataSindeni Wilayani Handeni.


Kamanda Mchunguzi amesema, Polisi wanaendelea kukusanya ushahidi wa kutosha ili kumfikisha Mahakamani Mtuhumiwa aliyetenda kitendo hicho kiovu.


Amewaasa wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao ili kuwaepusha na uwezekano wa kuingia kwenye vitendo vya watu wenye nia ovu kama vile makosa ya ubakaji na ulawiti.


Amesema,Wazazi na Walezi wanatakiwa kuhakikisha kuwa hata pale wanapowaacha watoto wao na wadada wa kazi wanakuwa katika mazingira yaliyokuwa salama.

Post a Comment

0 Comments