Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA BUNGE YAIPA MBINU MIKOA KUDHIBITI MICHANGO SHULENI

OR-TAMISEMI

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Denis Londo ametoa rai kwa mikoa yote nchini kuwa na mfano wa fomu maalumu ya wanafunzi kujiunga na masomo ya sekondari itakayodhibiti michango isiyo ya lazima.

Mhe. Londo ametoa rai hiyo kwenye ziara ya Kamati hiyo mkoani Iringa na kuonesha kufurahishwa na kile kinachofanyika katika mkoa huo kwa kuwa na fomu hiyo inayoonyesha kiwango cha mwisho cha michango kwa shule zote mkoani humo.

"Kipindi hiki cha kufungua shule na uandikishaji ukiwa unaendelea kuna baadhi ya maeneo kumekuwa na michango mingi na kila shule inajipangia na baadhi walimu wanashiriki kukiuka Sera na Miongozo ya Elimu hii si sawa ni vyema kila mkoa ukategeneza fomu maalumu kwa ajili ya kudhibiti michango,"amesema Mhe. Londo

Aidha, Kamati hiyo imetoa maelekezo mwanafunzi yeyote apokelewe na aingie darasani kama alivyo na asizuiliwe kusoma kutokana na kukosa michango wala sare ya shule na asome hadi hapo atakapoipata.

Naye,Mjumbe wa Kamati Mhe. Saashisha Mafue amesema hatua hiyo inasaidia wazazi wasibambikiwe michango mingi na kwamba jambo hilo ni la kuigwa.

Kamati hiyo imekamilisha ziara yake mkoani Iringa na kuelekea mbeya.

Post a Comment

0 Comments