Ticker

6/recent/ticker-posts

NEMC YASHIRIKIANA NA KITUO CHA SAYANSI NA MAZINGIRA INDIA KUTOA MAFUNZO YA UKAGUZI MAZINGIRA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya warsha Maalumu kwa Kushirikiana na kituo Cha Sayansi na Mazingira kutoka India (CSE India) yenye lengo la kutambua namna ya  mfumo wa ukaguzi wa mazingira unavyofanya kazi pamoja na kupeana uzoefu katika Usimamizi na Uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wahabari leo Januari 25,2024, Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka NEMC Bw. Novatus Mushi amesema kuwa mchakato wa usimamizi na Uhifadhi wa mazingira unahitaji uelewa mpana zaidi na taaluma mbalimbali ili kufanya ubobevu mkubwa katika ukaguzi huo.

"Ukaguzi wa mazingira lazima uhusishe wataalamu mbalimbali ili uweze kuzipata taarifa zote kwa ujumla wake ambazo utazihitaji kukuongoza katika ukaguzi wa mazingira ". Amesema Bw.Novatus.

Amesema kuwa NEMC wataendelea kujifunza kwa wageni wa mataifa mengine kwa kubeba mazuri ambayo wanayo na kuboresha katika huduma zao wanazotoa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Program ya Kupambana na Uchafuzi kutoka Viwandani Bw. Nivit Kumar wa Kituo Cha Sayansi na Mazingira India (CSE india) amesema kuwa anafikiri ni wakati sahihi kwa Mamlaka za Udhibiti wa Mazingira katika nchi za kiafrika kutumia ubunifu kuhifadhi mazingira ya nchi zao.

Aidha ameeleza kuwa walipofanya utafiti waligundua ripoti  za ukaguzi zilikuwa zikifanyika hazikuwa vizuri, hivyo wamejitahidi kuweka maelekezo vizuri jinsi ya kuchukua taarifa hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya (ECI) kutoka Kenya Bw. Gerphas Opondo amesema kuwa changamoto ya uchafuzi zilizopo Kenya na Tanzania ni zilezile, ijapokuwa Sheria za Uhifadhi zipo lakini watu bado wanakiuka taratibu hizo.

Warsha hiyo itafanyika kwa siku tatu na imejumuisha wadau mbalimbali kutoka mamlaka zinazosimamia mazingira kwenye mataifa mengine ya Afrika.

Post a Comment

0 Comments