Ticker

6/recent/ticker-posts

TPA YAIKABIDHI KAMPUNI YA ANOVA CONSULTING ENEO ITAKAPOJENGA BANDARI MBAMBA BAY

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA ) tarehe 27 Januari,2024 imeikabidhi rasmi kampuni ya Anova Consulting Company ltd eneo itakapojengwa Bandari ya Mbamba Bay iliyopo Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa Bw.Manga Gassaya amesema kampuni hiyo itasimamia ujenzi wa Bandari hii ili kuhakikisha kila kitu kinafanyika katika viwango na kukamilika kwa muda uliokubaliwa katika mkataba.

Aidha amesema kuwa kinachofanyika ni kumuonyesha msimamizi wa mradi (Anova Consult) mipaka ya eneo la ujenzi.

Makabidhiano hayo ni kufuatia mkataba wa usanifu na ujenzi wa uendelezaji wa Bandari ya Mbamba Bay uliosainiwa disemba 4,mwaka jana ambapo kampuni ya Xiamen Ongoing Construction Group Co ltd ndio itaendeleza ujenzi wa Bandari hiyo.

Post a Comment

0 Comments