Ticker

6/recent/ticker-posts

UTT AMIS YATOA SEMINA KWA WAANDISHI WA HABARI

KAMPUNI ya Uwekezaji ya UTT AMIS imetoa elimu kwa wahariri na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa jijini ikiwa ni hatua ya kuwasaidia kuelimisha umma kuhusu Uwekezaji.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo jijini hapa, ofisa mwandamizi kutoka kampuni hiyo, Rahimu Mwanga, amesema mafunzo hiyo yamekusudia kuwajengea uwezo kuhusu kuelimisha umma juu ya mifuko ya Uwekezaji wa pamoja.

"Tuna mifuko Sita ya Uwekezaji na tumekuwepo kwenye soko kwa takriban miaka 20 sasa na mifuko hii imekuwa ikifanya vizuri sokoni," amesema Mwanga.

Mwanga amesema mifuko hiyo ni pamoja na mfuko wa watoto, Umoja, Kujikimu, na Ukwasi, wekeza maisha na kwamba mpaka sasa wana zaidi ya wateja 300,000 huru rasilimali zao zikifikia thamani ya Sh1.9 trilioni.

Akieleza baadhi manufaa ya kuwekeza katika mifuko hiyo, Mwanga amesema wazazi na walezi wanaweza kutumia mfuko wa watoto kuwawekezea watoto wao ambao kiwango chake Cha Uwekezaji ni kidogo.

"Kuna watu Wana mahitaji ya kukuza mitaji kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi, kama vile biashara, kununua ardhi na kujenga, vyote hivi vinahitaji fedha, na fedha ya mkupuo inakuwa ni ngumu, kwa hiyo wanaweza kuanza kuwekeza kidogo na wakakuza mitaji kupitia mitaji yao," amesema.

Mwanga ameongeza kuwa kupitia mifuko ya hati fungani na mfuko wa kujikimu ambayo ni mifuko inayotoa magawio ya mara kwa mara, inalenga wawekezaji ambao wamepata hela za mkupuo kama wastaafu ambapoa inatoa gawio la mara kwa mara.

"Moja ya changamoto ya wastaafu ni namna nzuri ya kutumia mafao yao, kwahiyo kwa kupitia mfuko wa hati fungani wanaweza kuwekeza na kupata gawio kila mwezi au Kila baada ya miezi Sita," amefafanua.Post a Comment

0 Comments