Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA INDONESIA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe. Pahala Mansury jijini Jakarta, kwa ajili ya kuangalia hatua za mwisho za maandalizi ya Ziara ya Kitaifa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan itakayofanyika kuanzia tarehe 24-26 Januari, 2024 nchini humo.

Viongozi hao wamekubaliana kuwa maandalizi yote kwa ajili ya ziara hiyo yamekamilika na wako tayari kumpokea Mhe Rais tarehe 24 Januati atakapowasilo nchini Indonesia.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Waziri Makamba amesema ziara hiyo ni muendelezo wa Jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kayika kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Indonesia ambao mwaka huu unatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwake.

Ameongeza kuwa ziara hiyo pia inalenga kuimarisha Ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia katika maeneo ya kımkakati ya biashara, uwekezaji, Afya, elimu, uchumi wa buluu na kilimo.

Naye Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Mhe. Siregar amesema Indonesia iko tayari kumpokea Mhe Rais Samia nchini mwao na kuahidi kuwa Indonesia inauthamini uhusiano wake na Tanzania na itaendela kushirikiana kwa manufaa ya pande zote mbili.

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa na ziara ya Kitaifa nchini Indonesia kuanzia tarehe 24-26 Januari 2024.

Post a Comment

0 Comments