Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA ABSA TANZANIA YAWA MWANAHISA MPYA TMRC

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

TAASISI Maalum ya kifedha inayotoa mikopo ya muda mrefu kwa benki na taasisi za fedha kwa lengo la benki hizo na taasisi kutoa mikopo ya nyumba ya muda mrefu kwa wateja wao (TMRC) imeikaribisha benki ya ABSA Tanzania kama mwanahisa wake mpya.

Benki ya Absa imejiunga na TMRC kama mbia wa 19 kufuatia uwekezaji wa mtaji wa shilingi bilioni 1.62 ambapo benki hiyo inaungana na wanahisa wengine wa TMRC wa taasisi za fedha ikiwa ni pamoja na CRDB Bamk Plc, Benki ya NMB Plc, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) pamoja na benki na taasisi zingine za kifedha.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa TMRC, Bw. Oscar Mgaya amesema kuwa benki ya Absa kujiunga na TMRC, benki hiyo itaweza kupata fedha nyingi zaidi kwa madhumuni ya mikopo ya nyumba kutoka TMRC kama sehemu ya mkakati wake wa kukuza biashara yake kupitia utoaji wa mikopo ya nyumba.

Aidha amesema kuwa wanafurahi kuona benki nyingi zinajiunga na TMRC kwani kumekuwa na taasisi nyingi zaidi zikitoa mikopo ya nyumba .

"Mpaka sasa Tanzania kuna taasisi za fedha 31 ambazo zinatoa mikopo ya nyumba, leo Benki ya Absa amejiunga na TMRC na kufikia wanahisa 19, hivyo tunategemea taasisi nyingi kujiunga na TMRC na tunaendelea kuwashawishi wafanye hivyo". Amesema Bw. Mgaya.

Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Bw. Obedi Laiser amesema kuwa wamewekeza  Bilioni 1.6 kwa TMRC kwaajili ya kuboresha maisha ya watanzania kwa kuwapatia mikopo ya nyumba bora za  makazi kwa bei nafuu.

Amesema kuwa azma yao kuu ni kuiwezesha Afrika ya kesho kwaajili ya kuboresha maisha ya watu ambao ndio walengwa kwa kubadilisha maisha yao kupitia mikopo ya nyumba.

kuanzia kushoto, Mwenyekiti wa Bodi TMRC, Bw. Theobald Sabi, Mkurugenzi Mtendaji wa TMRC, Bw. Oscar Mgaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Bw. Obedi Laiser pamoja na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi Benki ya Absa, Bw. Richard Magongo wakikabidhiana hundi ya shilingi bilioni 1.62 ambazo zimetolewa na Benki ya Absa Tanzania kama mwanahisa mpya wa TMRC. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi TMRC, Bw. Theobald Sabi (kushoto) wakikabidhiana cheti na Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi Benki ya Absa, Bw. Richard Magongo mara baada ya benki ya Absa Tanzania kujiunga kama mwanahisa mpya TMRC. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi TMRC, Bw. Theobald Sabi akizungumza wakati wakiikaribisha benki ya Absa Tanzania kama mwanahisa mpya wa TMRC. Hafla hiyo imefanyika  leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa TMRC, Bw. Oscar Mgaya akizungumza wakati wakiikaribisha benki ya Absa Tanzania kama mwanahisa mpya wa TMRC. Hafla hiyo imefanyika  leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi Benki ya Absa, Bw. Richard Magongo akizungumza wakati wa hafla ya Benki ya Absa Tanzania kutangaza rasmi kujiunga na TMRC kama mwanahisa mpya. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Bw. Obedi Laiser akizungumza wakati wa hafla ya Benki ya Absa Tanzania kutangaza rasmi kujiunga na TMRC kama mwanahisa mpya. Hafla hiyo imefanyika leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa hafla ya kukaribishwa kwa benki ya Absa Tanzania kujiunga na TMRC iliyofanyika leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wakifuatilia hafla ya kuikaribisha benki ya Absa Tanzania kujiunga na TMRC iliyofanyika leo Februari 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)Post a Comment

0 Comments