Ticker

6/recent/ticker-posts

Kamishina Wakulyamba - Tumieni vita ya Majimaji kukuza Utalii wa Utamaduni

Na John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishina Benedict Wakulyamba ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa Utalii na utamaduni kuanzisha makumbusho ya vita vya Majimaji ili kupata zao jipya la Utalii wa Utamaduni katika ukanda wa kusini mwa Tanzania.

Kamishina Benedict Wakulyamba ametoa wito huo leo Februari 27, 2024 wakati akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki kutoa hotuba ya kufunga Tamasha la Majimaji mjini Songea kwenye viwanja vya makumbusho ya vita vya Majimaji.

Wakulyamba amefafanua kuwa tayari Serikali imefanya marekebisho ya Sera ya Malikale na kuwaruhusu wawekezaji kuwekeza katika kuanzisha makumbusho.

Aidha, Wakulyamba amesisitiza kuwa Tamasha la Majimaji limeendelea kutumika katika kuenzi amani na mshikamano wa jamii nzima ya kitanzania ambayo tumeachiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Karume.

Pia amesema Wizara inaendelea kushirikiana na Wilaya ya Kilwa kufanya Tamasha katika eneo la Nandete ambako vita ilianzia.

Ametaja baadhi ya mikakati mingine ambayo wizara inafanya ni kuendelea kubaini maeneo yaliyotumika na vita vya Majimaji katika mikoa Saba ya kusini mwa Tanzania, kufanya mabadiliko ya Sera ya Malikale na kubaini maeneo, kukarabati na kuyatangaza katika gazeti la Serikali kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.

Pia kuruhusu watu binafsi kuanzisha makumbusho binafsi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha mchakato baina ya Serikali ya Tanzania na Ujerumani wa kurejesha mabaki ya machifu na kulipa fidia.

Aidha, amesema historia ya Tanzania haiwezi kukamilika bila vita ya majimaji na kwamba mashujaa wa vita ya Majimaji walipanda mbegu ya mshikamano, amani na upendo kwa nchi ya Tanzania.

Vita ya Majimaji ilianza mwaka 1905-1907 na ilijumuisha jamii 21 katika mikoa 7 ya kusini mwa Tanzania ambapo mashujaa 67 wa vita walinyongwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja wakati wakipigania uhuru wao.

Katika Tamasha hili Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amezindua kitabu kiitwacho Masimilizi wa vita ya Majimaji kinachoelezea vita ilivyopigwana katika maeneo ya Upangwa.

Tamasha hili lilijumuisha wadau mbalimbali kutoka Malawi, na wadhamini pia lilipambwa na vikundi vya sanaa za Ngoma vya Mhamba , umoja na Shamba sanaa kutoka

Post a Comment

0 Comments