Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU DKT. KIDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA IDARA YA MASUALA YA UCHUMI KUTOKA EU

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida leo tarehe 15 Februari, 2023 jijini Dar es salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya masuala ya Kiuchumi (Head of Governance and Economic Section) kutoka Umoja wa Ulaya (EU) Bi. Karina Dzialowska na kujadiliana kuhusu namna wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kuibua mikakati mbalimbali inayolenga kuongeza uwekezaji nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiuchumi, Bi. Karina alimhakikishia Dkt.Kida kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Aidha, Bi. Karina alibainisha uwepo wa fursa ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uwekezaji katika miradi rafiki kwa mazingira (Green investment) ambayo itatokana na fedha zinazopatikana kupitia Masoko ya mitaji kwa Amana mahsusi kwa ajili ya miradi rafiki kwa mazingira (Green Bonds).

Vilevile, katika kikao hicho viongozi hao wamezungumzia utekelezaji wa Mpango wa Maboresho ya mazingira ya Biashara na Uwekezaji BLUEPRINT unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Business Environment Growth Innovation (BEGIN).

Post a Comment

0 Comments