Ticker

6/recent/ticker-posts

MAJALIWA: SHILINGI MILIONI 920 KUJENGA SHULE MBILI ZA SEKONDARI RUANGWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa sh milioni 920 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili za Sekondari ikiwemo za Namakuku na Namichinga, Wilayani Ruangwa ikiwa ni muendelezo wake wa koboresha sekta ya elimu nchini.

Amesema ujenzi wa Shule hiyo utasaidia wanafunzi katika maeneo hayo kutotembea umbali mrefu kufuata shule “Nawapongeza sana wakazi wa Namakuku kwa uamuzi wenu wa kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule, huku ni kumuunga mkono Rais Dkt. Samia”

Amesema hayo leo Jumanne (Februari 20, 2024) wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Zahanati Namakuku pamoja na Taa za barabarani kwenye kata ya Chienjele, Ruangwa Mkoani Lindi.

Akizungumza kuhusu ujenzi wa Zahanati hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa zahanati ambayo ni jitihada za Wananchi pamoja na Ofisi ya Mbunge ina vyumba vyote muhimu “Mmejenga jengo kubwa lenye vyumba vingi vyenye hadhi ya kituo cha Afya, mganga mkuu wa wilaya amekagua na amegundua linafaa kuwa kituo cha afya kidogo”

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, Wilaya ya Ruangwa imepata mabadiliko makubwa katika sekta zote za maendeleo “Niliamua kuwaita viongozi wa Chama cha Mapinduzi ili wasikie mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hapa Ruangwa “lazima tumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ametufanyia mambo makubwa sana”

Wakizungumza katika mikutano hiyo Diwani wa Kata ya Chienjele Rashidi Nnunduma na Diwani wa Viti Maalum wa Kata hiyo Dalini Mbira, wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoomgozwa na Rais Dkt . Samia kwa miradi ya meendeleo kwenye sekta za maji, kilimo, elimu, afya na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments