Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MNDEME AONGOZA SHEREHE ZA POLISI 'POLICE DAY' SHINYANGA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati) akicheza na Wasalama (Jeshi la jadi Sungusungu kutoka Chibe - Shinyanga)
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Sherehe ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Februari 3,2024 katika Viwanja wa Polisi Kambarage Mjini Shinyanga
Askari polisi waliopewa pongezi na zawadi kwa kufanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023

-Askari polisi waliofanya vizuri zaidi wapewa zawadi

-Ataka Kasi Usimamizi Sheria Kudhibiti Ajali barabarani

-‘Madada Poa na Makaka Poa , Wahalifu wakafanye shughuli Nyingine

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameongoza askari wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kusherehekea sikukuu ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ yenye lengo la kuwaleta askari polisi na familia zao, jamaa na marafiki ili kufurahi na kubadilishana mawazo na mikakati ya kiutendaji.

Sherehe za Police Day zimefanyika leo Jumamosi Februari 3,2024 katika Viwanja vya Polisi Kambarage Mjini Shinyanga na viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa dini, jeshi la jadi sungusungu Chibe, askari polisi, wananchi na wadau mbalimbali.

Akizungumza wakati wa Sherehe hizo, baada ya gwaride lilioambatana na ugawaji vyeti na zawadi kwa askari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewapongeza askari polisi kwa kazi kubwa wanayofanya katika kulinda Amani na usalama wa mkoa wa Shinyanga.

“Shinyanga ipo salama, Shinyanga imetulia kutokana na kazi kubwa inayofanywa na askari polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi. Mmejipanga vizuri, askari wana ari na uzalendo wa kutosha kukabiliana na uhalifu na wahalifu. Nimeona mazoezi yenu ya utayari na gwaride kwa kweli wote mnafanya kazi nzuri, lakini waliofanya vizuri zaidi tumewapatia vyeti vya pongezi”,amesema Mhe. Mndeme.

“Jeshi la Polisi Shinyanga lipo imara, wahalifu mliopanga kufanya uhalifu hiyo nafasi haipo Shinyanga”,ameongeza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme

Aidha amewataka askari polisi kuendelea kuchukua hatua za kudhibiti wahalifu na uhalifu, kutumia vyombo vya habari kutoa elimu ya kuzuia uhalifu huku akiwakumbusha wananchi kutoa taarifa za matukio ya uhalifu na wahalifu ili mkoa wa Shinyanga uendelee kuwa salama.

“Kama kuna Madada poa basi kuna makaka poa, Hao wanaouza miili yao hawana nafasi Shinyanga. Tutaendelea kudhibiti biashara hiyo kwani ni kinyume cha maadili yetu, askari polisi timizeni wajibu wenu . Wale watu wanaofanya biashara ya kuuza miili naomba wakafanye shughuli nyingine kwani kuuza miili inavunja na kukiuka maadili ya jamii yetu. Tutaendelea kuchukua hatua”,amesema Mndeme.

Kuhusu ongezeko la ajali za mara kwa mara, Mhe. Mndeme amewataka askari wa kikosi cha usalama barabarani kuongeza kasi ya kusimamia sharia za usalama barabarani huku akiwataka madereva kutii sharia za usalama barabarani lakini pia watumiaji wa barabara kuchukua tahadhari pindi wanapoingia barabarani.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limeteua siku moja ili kuwaleta pamoja familia za polisi, jamaa na marafiki ili kusherehekea pamoja , kufurahi na kubadilishana mawazo na mikakati ya utendaji kwa kipindi cha mwaka unaoanza wa 2024.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi

“Kwa ujumla askari wengi wanafanya kazi vizuri katika majukumu yao. Kwa kurejea muongozo wa Jeshi la Polisi (P.G.O) K/F Na. 37 (1) – 11 unaotutaka kumpongeza askari polisi aliyefanya kazi vizuri zaidi katika utendaji wake wa kazi, tuliweza kuwapendekeza askari wachache ambao tunadhani walifanya vizuri zaidi katika majukumu yao kwa kipindi cha mwaka 2023, tunawapatia pongezi na zawadi ili waweze kuongeza juhudi na tija katika utendaji wao kwa siku zijazo”,ameeleza Magomi.

Amezitaja baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kuwa ni uhaba wa vitendea kazi yakiwemo mafuta ya magari, uchakavu wa magari, uchache wa fedha za matengenezo ya miundombinu mfano magari, ofisi na nyumba za askari.

Aidha ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa ushirikiano inaoutoa katika kutekeleza majukumu ya jeshi la Polisi Shinyanga ikiwemo kulipatia rasilimali vifaa kama gari aina ya Toyota Land Cruiser iliyotoa hivi karibuni kwa ajili ya Kikosi cha kutuliza ghasia Polisi Mkoa wa Shinyanga.

Sherehe za Police Day zimeambatana na burudani mbalimbali.

TAZAMA VIDEO Jeshi la Jadi la Sungusungu Likitoa Burudani..Mkuu wa Mkoa ashindwa kuvumilia, Ainuka

ANGALIA PICHA  MATUKIO YALIYOJIRI HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa Sherehe ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Februari 3,2024 katika Viwanja wa Polisi Kambarage Mjini Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa Sherehe ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ Mkoa wa Shinyanga leo Jumamosi Februari 3,2024 katika Viwanja wa Polisi Kambarage Mjini Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikagua Gwaride wakati wa Sherehe ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ Mkoa wa Shinyanga

Gwaride wakati wa Sherehe ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ Mkoa wa Shinyanga
Gwaride wakati wa Sherehe ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ Mkoa wa Shinyanga
Gwaride wakati wa Sherehe ya Polisi na familia zao ‘Police Family Day’ Mkoa wa Shinyanga
Askari polisi waliopewa pongezi na zawadi kwa kufanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akikabidhi cheti na zawadi kwa mmoja wa maaskari polisi waliofanya kazi vizuri zaidi mwaka 2023
Askari polisi wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Askari polisi wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi wakicheza na Wasalama (Jeshi la jadi Sungusungu kutoka Chibe - Shinyanga)
Ngoma ya Wagoyangi ikiendelea 
Ngoma ya Wagoyangi ikiendelea , jamaa anacheza na nyoka. Kushoto ni MC Mzungu Mweusi
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) wakiteta jambo
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wananchi na askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Meza kuu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Wananchi na askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Askari polisi na wananchi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
MC Tumaini akiwa eneo la tukio
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) 
Askari polisi wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Askari polisi wakionesha onesho la Mbwa waliopewa mafunzo maalum
Oscar Nyerere akitoa burudani
Askari polisi maarufu Nyumbu Mjanja akitoa burudani
Wananchi wakifuatilia burudani

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments