Ticker

6/recent/ticker-posts

WHO, SERIKALI YA IRELAND NA USWIZI WASAINI MAKUBALIANO KUFANYA MPANGO MKAKATI WA KISEKTA-V (HSSP V)

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO), Serikali ya Ireland na Uswizi wametia saini makubaliano ya kufanya Mpango Mkakati wa Kisekta-V (HSSP V) wa kuimarisha mifumo ya afya nchini Tanzania.Chini ya makubaliano hayo Serikali za Ireland na Uswizi zitatoa kwa pamoja Sh. 258 milioni kwa kusudi hilo.

Mpango mkakati huo uliandaliwa na Wizara ya Afya ikishirikiana na wadau wa maendeleo na Taasisi zisizo za kiserikali mwaka 2019 ikiwa na kauli mbiu ya kutomuacha mtu nyuma.

Akizungumza leo Februari 28,2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo, Mwakikishi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt Charles Moses kwa niaba ya Wizara ya Afya Tanzania amesema mapitio ya mpango huo hufanyika kila baada ya mwaka mmoja na nusu na unatoa mwanya wa kufanya mapitio kama vipaumbele vyote katika sekta ya afya vinatekelezwa.

Amesema mapitio hayo yataangalia matokeo ya utekelezaji wa mpango huo kwenye utoaji wa huduma za afya, uwekezaji kwenye sekta hiyo na kutengeneza njia ya uwepo wa mpango mkakati wa sita wa wizara hiyo.

"Fedha hizi si tu zitakwenda kuboresha mfumo wa afya uliopo ambao kwa kiwango kikubwa WHO imeshirikishwa bali kuondoa miaya iliyopo kwenye utekelezaji wa mpango". Amesema Dkt. Moses

Kwa upande wake Mwakikishi Ubalozi wa Uswis, Holgrr Tausch aliwahamasisha wadau wa maendeleo kuendelea kuunganisha nguvu pamoja kutekeleza vipaumbele vya taifa na kuongozwa na ushahidi unaopatikana kwenye mapitio ya mpango huo.

Nae Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland Mary amesema anatambua mafanikio yaliyofikiwa na Serikali kwenye sekta ya afya ikiwemo kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia SDGs hasa lengo la tatu kuwa na Afya bora na lengo la tano la usawa wa kijinsia.

Aidha amesema Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto pamoja na Viashiria vya Malaria yam waka 2022 umerekodi mafanikio makubwa katika viashiria vya afya ikiwa ni pamoja na kupungua kwa vifo vya uzazi, vifo vya watoto chini ya miaka mitano na udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza.

Pamoja na hayo amesema Mpango Mkakati wa tano wa Sekta ya Afya unaweka dira ya huduma ya afya nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2021 hadi 2026.

Post a Comment

0 Comments