Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI DKT. NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU WA KANISA LA NGLCC MKOANI MARA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Ndugu Kassim Majaliwa Majaliwa, alipowasili kushiriki shughuli ya mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NGLCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Fransisca Mwita Gachuma, yaliyofanyika Jumamosi, Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime Vijijini. Askofu Fransisca alikuwa mwenza wa Ndugu Christopher Mwita Gachuma, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, kutokea Mkoa wa Mara.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na kuzungumza jambo na Askofu Mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Dkt. Daniel Ouma (mwenye joho), mara baada ya misa ya kumuombea marehemu, kabla ya mazishi ya Askofu wa NGLCC, Jimbo la Mara Kaskazini, Fransisca Mwita Gachuma, yaliyofanyika Jumamosi, Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime Vijijini. Askofu Fransisca alikuwa mwenza wa Ndugu Christopher Mwita Gachuma (kushoto mwenye suti), ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, kutokea Mkoa wa Mara. Wengine wanaofuatilia ni viongozi wa Kanisa la NLGCC).
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akishiriki utoaji wa heshima za mwisho, kumwaga mchanga na kuweka shada la maua, wakati wa mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, marehemu Fransisca Mwita Gachuma, yaliyofanyika Jumamosi, Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime Vijijini. Askofu Gachuma alikuwa mwenza wa Ndugu Christopher Mwita Gachuma, ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, kutokea Mkoa wa Mara. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Taifa, Komredi Mary Pius Chatanda. Kushoto pichani anayeangalia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Halima Mamuya na aliyeko kulia pichani akiangalia ni Mhe. Christina Mndeme, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Muungano na Mazingira), wakati wa kushiriki msiba wa marehemu Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Fransisca Mwita Gachuma, huko Komaswa, Tarime vijijini, mkoani Mara, Jumamosi, Machi 30, 2024.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi akifurahia jambo wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Issa Haji Usi Gavu (katikati), ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Taifa, Oganaizesheni (katikati) na Ndugu Dk. Frank Haule Hawassi, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha (kulia), mara baada ya misa ya kumuombea marehemu, wakati wa mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Marwa Kaskazini, Fransisca Mwita Gachuma, Jumamosi, Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime vijijini, mkoani Mara. Askofu Gachuma alikuwa mwenza wa Ndugu Christopher Mwita Gachuma, Mjumbe wa NEC ya CCM Taifa, kutokea Mkoa wa Mara.
Sehemu ya umati wa waombolezaji wakishiriki misa ya kumuombea marehemu, wakati wa mazishi ya Askofu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church (NLGCC), Jimbo la Mara Kaskazini, Fransisca Mwita Gachuma, Jumamosi, Machi 30, 2024, huko Komaswa, Tarime vijijini, mkoani Mara. Askofu Gachuma alikuwa mwenza wa Ndugu Christopher Mwita Gachuma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Taifa, kutokea Mkoa wa Mara.

Post a Comment

0 Comments