Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI KASIKE AFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA AFYA WA MSUMBIJI MHE. ARMINDO TIAGO

Mhe Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Msumbiji alikutana na Prof. Armindo Tiago, Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Msumbiji tarehe 20 Machi 2024 kwenye Ofisi za Wizara ya hiyo zilizopo Jijini Maputo.

Wakati wa Mkutano huo, Viongozi hao wawili walizungumza masuala mbalimbali ya Ushirikiano katika Sekta ya Afya ikiwemo pendekezo la kusainiwa Hati ya Makubaliano (MoU) itakayowezesha Tanzania kuuza Madawa na Vifaa Tiiba nchini Msumbiji.

Aidha, Viongozi hao walizungumza pendekezo la Tanzania la kutuma Timu ya Wataalam wa Afya watakaoweka kambi nchini Msumbiji kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wenye matatizo ya moyo.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania - Maputo

20 Machi, 2024

Post a Comment

0 Comments