Ticker

6/recent/ticker-posts

BF SUMA YAZINDUA TAWI KAHAMA, YAANIKA FURSA KWA WANANCHI


Kiongozi wa Ofisi ya BF SUMA, Juma Mwesigwa akizungumzia fursa zinazopatikana BF SUMA


Na Neema Nkumbi Huheso Digital & Huheso Fm

Kampuni ya Bright Future Superior Unique Manufacturer of America (BF SUMA) imezindua rasmi tawi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ambapo wananchi wametakiwa kuchangamkia fursa zinazopatikana katika kampuni kwa maendeleo yao na jamii kwa ujumla.


Akizungumza leo Jumamosi Aprili 20,2024 wakati wa uzinduzi wa tawi la BF SUMA tawi la Kahama, Kiongozi wa Ofisi ya BF SUMA, Juma Mwesigwa amesema BF SUMA inajihusisha na utafiti wa shida za kiafya , uzalishaji wa bidhaa za afya
na sambazaji wa bidhaa za kiafya hivyo kuiomba jamii kuchangamkia fursa zilizopo katika kampuni hiyo.


Kwa upande wa usambazaji BF SUMA inatoa ajira kwa watu bila kujari kiwango elimu walichonacho ambapo tayari imetengeneza ajira za watu zaidi ya 3,000 nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Kiongozi wa BF SUMA Kanda ya Ziwa Dkt. Daniel Limbu amesema malengo makubwa ya Kampuni hiyo ni pamoja na kufanya tafiti juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa, kukuza uchumi kupitia ajira ambapo inamuwezesha mwanachama kuuza dawa hizo na kusambaza kwa wagonjwa na kujali afya za watumiaji wa dawa hizo kupitia matibabu yanayotolewa na kampuni hiyo.
Naye Kiongozi  wa BF SUMA Tanzania, Kambarage Samwel amepata nafasi ya kuzungumza akitoa ushuhuda wa dawa zinazotokana na kampuni hiyo na kusema kuwa kupitia dawa hizo ameokoa maisha ya baadhi ya watu akiwemo mama yake mzazi.

''... Nakumbuka tulimpoteza baba mzazi wakati tunahangaika kuchangisha kwa wadau kulingana na hali ngumu ya kiuchumi tuliyokuwa nayo katika familia na wakati anafariki baba yetu tulikuwa tumefikisha 780,000/=  badala ya milioni tatu na laki tatu kama gharama ya matibabu, pesa ambazo badala ya kufanya matibabu ya baba mzazi zilitumika katika mazishi yake, lakini kwa hali ya afya ya mama yangu mzazi hakuna ambaye angejua kama mpaka sasa angekuwa hai lakini kupitia BF SUMA bado ni mzima'', amesema Kambarage.

Amesema ni dhahiri shahiri kuwa wakati fursa hii inafungua dunia kwa vijana wengi duniani Dkt Rose ni mmojawapo wa vijana ambao wamebadilishiwa maisha yao kupitia kampuni hii na kuwabadilishia maisha watu wengine pia.


''... Nakumbuka pale Dar es salaam kuna dada wa kazi nilikutana naye ambaye aliingia Dar es Salaam akiamini kuwa atafanikiwa kuikwamua familia yake kutokana na hali duni ya maisha ya familia yao lakini haikuwa hivyo na nilipokutana naye nikamshirikisha fursa hii aliweza kunielewa na akajiunga na kampuni hii ambapo mpaka sasa amekuwa ni tegemezi katika familia yao'',ameeleza.

Kampuni ya BF SUMA ni kampuni ambayo inafanya kazi kwenye mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Australia, Africa Kusini na mataifa mengine na ni kampuni ambayo inakuruhusu kutengeneza kipato chako cha ziada mbali na ile ajira ya msingi na ni kampuni yenye mafanikio makubwa tangu ilipoanzishwa mnamo mwaka 1993 huko barani America, Los Angeles.

Post a Comment

0 Comments