Ticker

6/recent/ticker-posts

CHIKOTA ALIA UHABA WA WATUMISHI NANYAMBA


MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota,akichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI 2024/25 bungeni jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu, DODOMA

MBUNGE wa Jimbo la Nanyamba Abdallah Chikota amempongeza Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kongani ya viwanda vya kubangua korosho mkoani Mtwara.

Alitoa pongezi hizo jana bungeni jijini hapa wakati wa mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI 2024/25, alisema kongani hiyo itasaidia uzalishaji wa ajira kwa wakazi wa mkoa huo.

“Tunamshukuru Rais kwa mradi wa umwagiliaji wa Arusha chini, ujenzi wa viyuo vya afya vitatu, mradi wa TACTIC, ujenzi wa stendi mpya ya mabasi na ujenzi wa barabara ya lami kilomita tano,” alisema Chikota.

Alimpongeza Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa na Manaibu Waziri wake kwa uchapakazi wao na kushughulikia hoja za wabunge.

Hata hivyo, alisema jimboni kwake yapo matatizo yanayohisiana na miundombinu ambapo mbali na kuupungeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) alisema wakala huo unakabiliwa na upungufu wa Wahandisi wa barabara.

Alisema meneja wa TARURA katika jimbo lake anahudumia wilaya tau ambazo ni Masnispaa ya Mtwara, Halmashauri ya Mtwara na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba.

Alipendekeza kuwa TAMISEMI ipewe kibali maalum cha kuajiri Wahandisi wa barabara kwaajili ya kupelekwa wilayani.

Alisema upungufu wa watumishi pia upo katika sekta ya afya ambapo katika mkoa wa Mtwara kuna upungufu wa 6.088 waliopo ni 2,153 ambao ni upungufu wa asilimia 65.

Katika sekta ya elimu alisema kuna upungufu wa walimu ambapo aliishauri TAMISEMI kuhakikisha inatoa kibali cha walimu 300 kuajiriwa katika Halmashauri ya Nanyamba.

Alisema mapato ya serikali za mitaani madogo na vyanzo vingi si vya ukakika na vichache vilivyopo havisimamiwi vizuri.

“Halmashauri nyingi zinategemea ushuru wa mazao kama chanzo muhimu cha mapato yake. Vyanzo vingi vya uhakika vipo serikali kuu,” alisema Chikota.

Alisema kwasababu wizara imetenga Zaidi ya Sh. Bilioni 190 kwaajili ya ununuzi wa magari ya viongozi basi Mkuu wa Wilaya ya Mtwara anunuliwe gari jipya kwasababu lililopo halimwezeshi kutimiza majukumu yake vizuri.

Post a Comment

0 Comments