Ticker

6/recent/ticker-posts

HOSPITALI YA HEAMEDA YAZINDUA MTAMBO WA KISASA KUTIBU MARADHI YA MOYO

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

HOSPITALI ya Heameda,imezindua Maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha.

Akizungumza April 18 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mtambo huo ambao ni lulu nchini katika taratibu za matibabu ya moyo, Mkurugenzi wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Meshack Mwandolela alisema hospitali iliamua kuitenga siku ya April 18,2024 kwa ajili ya vipimo vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na moja wapo ya magonjwa hayo ni ugonjwa wa  moyo na wameibaini watu wengi wanasumbuliwa na maradhi hayo na hawakujua kwasababu hayaoneshi dalili.

Aidha Dkt.Mwandolela alisema mtambo huo unawasaidia kuweka vifaa maalumu kusaidia wagonjwa  wa moyo ambavyo ni pacemaker vinavyowekwa kwenye moyo kwa ajili ya kusaidia mambo mbalimbali.

"Mojawapo ya magonjwa yanayotibiwa kwa pacemaker ni wale wenye moyo unaoenda taratibu na wale wanaopata milipuko ya moyo bila mpangilio na Kuna wengine wanapata moyo mkubwa,na kushindwa kufanya kazi kwahiyo tunawawekea pacemaker maalumu ambayo inasaidia kupunguza saizi ya moyo,lakini pia kuongea nguvu ya moyo kusukuma damu"Mwandolela alisema

Aidha Dkt.Mwandolela alieleza kuwa tangu wameweka mtambo wa CATH LAB wamefanikiwa kufanya vipimo kwa wagonjwa  zaidi ya  15 pamoja na kuweka pacemaker kwa wagonjwa takribani watatu vilevile na kwa wagonjwa watatu ambao walikua na changamoto ya kuziba kwa mishipa inayokwenda kwenye moyo.

"Tumeweza kuokoa gharama kubwa sana, kwa ajili ya matibabu haya mtu huyu ambaye alikua anatakiwa asafiri kwenda India anakuwa ameokoa pesa na muda kwa wanaomuuguza kwahiyo tunapunguzaa gharama kubwa ili watu waweze kufanya mambo yao mengine wakiwa hapa" alieleza Dkt.Mwandolela

Pamoja na hayo ametoa rai kwa wananchi kutoogopa matumizi ya teknolojia za kisasa ambazo zilichelewa kuingia nchini ,na zimekuwa zikitumika huko katika mataifa ya kigeni kwa muda mrefu ambapo imechangia kuokoa maisha na watu kuishi kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt.Gunini Kamba, ameipongeza Hospitali ya Heameda kwa kufunga vifaa Bora ambavyo vinafanya huduma za kibingwa kwa kuzibua mishipa iliyoziba kwenye moyo.

"Mashine iliyofungwa ni ya kisasa sana ,katika nchi yetu zipo tano,na ukizingatia ina uwezo wa kuzibua mishipa ya moyo, tunashukuru tuna JKCI inafanya huduma hiyo lakini peke yake haijitoshelezi", alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe alionesha kujivunia timu yao ya watendaji katika hospitali hiyo kwa uadilifu wao kazini pamoja na juhudi katika shughuli  zao kupambania kutoa huduma bora.

Vilevile Madaktari kutoka India walieleza kuwa watashiriki kuziba nafasi iliyokuwa wazi nchini kwa  kutoa huduma za kibingwa katika matibabu ya ugonjwa wa moyo kwa wagonjwa ambao wamechelewa kupata huduma hiyo ya upasuaji wa moyo (Cardiac Surgery).

Heameda imejikita hasa katika huduma za kitabibu katika magonjwa ya moyo, saratani, pamoja na kuchuja damu kwa wagonjwa wa figo iliyofeli ambapo wamelenga kusaidia wananchi kupunguaza gharama kufata matibabu nje ya nchi.

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Gunini Kamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka nchini Inida akizungumza wakati wa uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akieleza jambo kwa wadau mbalimbali walioshiriki katika hafla ya uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.
Sehemu maalumu ya kuwalaza wagonjwa mara baada ya kufanyiwa matibabu katika Hospitali ya Heameda iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya madaktari bingwa pamoja na wadau mbalimbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa maabara yenye mtambo wa kisasa unaoshughulika na masuala ya matibabu ya moyo (Cardiac Catheterisation Labatory) ambao unachukua picha na kumwezesha Daktari kuingia ndani ya moyo na kuchunguza mishipa ya damu iliyoziba na kuzibua mishipa hiyo pamoja na kusaidia kuchunguza presha. Hafla hiyo imefanyika April 18 2024 kwenye hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments