Ticker

6/recent/ticker-posts

LHRC YATOA TAARIFA YA UCHAMBUZI KUHUSU SHERIA YA UCHAGUZI

KITUO Cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kimetoa wito kwa Serikali kuwasilisha mswada wa sheria utakaotoa fursa ya kufanya mabadiliko ya katiba ili kuruhusu baadhi ya maswala ambayo kwa uasilia wake hayawezi kufanyiwa marekebisho bila kugusa katiba.

Hayo yamewasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Wakili Anna Henga wakati akitoa taarifa ya uchambuzi wa kituo hicho kuhusu sheria ya uchaguzi baada ya kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuna haja ya kufanywa marekebisho ya sheria ya uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani 2024 ili kuweka takwa la ulazima wa kufanya midahalo ya wagombea katika ngazi zote.

Ameendelea kwa kubainisha kuwa maoni ya wadau juu ya mgombea binafsi yameachwa na hayajachukiliwa kwa uzito unaotakiwa licha ya kuwepo kwa maamuzi mbalimbali ya mahakama za ndani na kikanda ambazo zimetoa maamuzi ya kuwepo kwa mgombea binafsi lakini bado kumekuwepo na kusita kufanywa maamuzi ya kurekebisha katiba na sheria.

"Kwa mujibu wa vifungu vya 32,55 na 60 vya sheria ya uchaguzi wa Rais , wabunge na madiwani 2024,moja ya sifa mtu kuchaguliwa kuwa Rais,mbunge au diwani ni lazima awe anatokana na chama cha siasa, hii inathibitisha kutochukuliwa kwa maoni ya wadau tuliotaka uwepo wa mgombea binafsi, licha ya LHRC na wadau wengine kupendekeza mabadiliko madogo ya katiba katika ibara za 67(1)(b) na 39(1)(c) za katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ili kuruhusu uwepo wa mgombea binafsi lakini bado Serikali halijalifanyia kazi"

Ameendelea kwa kusema kuwa "ni imani yetu kwamba, uwepo wa mgombea binafsi utachochea ukuaji wandemokrasia pamoja na kuongeza wigo wa watanzania kuwa na haki ya kuchaguliwa bila kulazimika kupitia mkondo wa vyama vya siasa".

Akizungumzia uchambuzi wa masuala yaliyoachwa kwenye sheria ya uchaguzi wa Rais,wabunge na madiwani no 2. 2024 amesema"miongoni mwa mambo ambayo LHRC na wadau wengi tulishauri ni tume kuajiri watumishi wake yenyewe ili kuipa uhuru wa kutosha katika utelekezaji wa majukumu yake na kuongeza uaminifu kwa wadau wa uchaguzi. Pendekezo hilo halikuchukuliwa badala yake watumishi wa umma wameendelea kuwa sehemu ya tume".

Post a Comment

0 Comments