Ticker

6/recent/ticker-posts

MAANDALIZI YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024 YAKAMILIKA

Na; Mwandishi Wetu – Kilimanjaro

Serikali imesema kuwa shughuli za maandalizi kuelekea kuzindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 zakamilika.

Amesema hayo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Tabia Mwita, leo tarehe 1 Aprili, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa mwenge huo.

Aidha, WAZIRI Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru 2024 Kitaifa zitakazofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), tarehe 2 Aprili, 2024, Mkoani Kilimanjaro.

Amesema baada ya uzinduzi mwenge huo utakabidhiwa kwa vijana sita kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuukimbiza katika mikoa 31 yenye jumla ya halmashauri 195 za Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa siku 195.

Kwa upande wengine, Mhe. Tabia Mwita amesema kwa kipindi chote cha kuukimbiza Mwenge wa Uhuru utafanya kazi ya kuhamasisha amani, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa pamoja na kuwahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao.

Ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni “Kutunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Mhe. Tabia Mwita akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru leo Aprili 1, 2024, Mkoani Kilimanjaro. Katikati ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kushoto) akieleza jambo  Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Watendaji kutoka ofisi yake na Kamati mara baada ya kukagua hatua za maandalizi ya uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), Mkoani Kilimanjaro.
Sehemu ya vijana wa Halaiki wakiwa katika mazoezi kwenye uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), kuelekea uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kilimanjaro.

Post a Comment

0 Comments