Ticker

6/recent/ticker-posts

MATUKIO KATIKA PICHA OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bi. Mary Maganga pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa bungeni tarehe 15 Aprili, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha Sita unaoendelea Bungeni, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi (wa pili kutoka kushoto), Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga (wa kwanza kulia) Bungeni leo tarehe 15 Aprili, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Bunge, Kikao cha Sita.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Mary Maganga akutambulishwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa 15 wa Bunge, kikao cha Sita, bungeni jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili, 2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Boniface Simbachawene, Bungeni jijini Dodoma leo Aprili 15, 2024.

Post a Comment

0 Comments