Ticker

6/recent/ticker-posts

MIRADI YA SH BILIONI 11 KUFIKIWA NA MWENGE WA UHURUJIJINI TANGA


Na Hamida Kamchalla, TANGA.


MIRADI 8 yenye zaidi ya sh bilioni 11 itapitiwa na mbio za mwenge wa uhuru jijini Tanga kesho aprili 14, ambapo utakimbizwa km 99.3, katika tarafa 4, kata 14 na mitaa 81 katika jiji hilo.


Mwenge wa Uhuru utahamasisha shuhuli mbalimbali za wananchi, ikiwemo serikali za mitaa, lakini pia mapambano dhidi ya vvu, malaria, dawa za kuleya, rushwa pamoja na uhamasishaji wa lishe bora.


Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji akitoa taarifa ya ujio wa mbio za mwenge huo ofisini kwake, amesema mara baada ya mapokezi utakagua namna halmashauri hiyo inavyotunza mazingira na kudibiti taka ngumu katika dampo la Mpirani na kupanda miti 50 ya matunda.


Aidha amebainisha mwenge utafungua mradi wa maji mtaa wa Putuni wenye thamani ya takribani sh bilioni 2, lakini pia utakagua miti 300 iliyopandwa wakati wa mapokezi ya mwenge mwaka jana katika shule ya sekondari Kiomoni.


"Mwenge wa Uhuru utatembelea kituo cha watu wenye mahitaji maalumu cha YDCP kilichopo kata ya Central ambacho kilipewa wataalamu wanne na halmashauri ya jiji ikiwa ni juhudi za kushirikiana na wadau katika kuibua na kuwasaidia watu hao,

"Lakini pia utapokea taarifa ya halmashauri inavyopambana na dawa za kulevya pamoja na kutembelea shuhuli za vijana ambao wamekopesha sh milioni 20 katika kituo cha kuoshea na ukarabati mdogo wa magari (Mkwakwani Youth Centre),

"Pia utazindua mradi wa ufuaji wa umeme wa jua kwenye kiwanda cha uzalishaji wa mifuko cha PPTL, ambao una thamani ya sh bilioni 6.7" amesema Kaji.

Amesema kuna vyumba vinne vya madarasa katika shule ya msingi Majengo vyenye thamani ya sh milioni 100 vitafunguliwa, ikiwa ni pamoja na kupokea taarifa ya lishe na mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI katika halmashauri hiyo.


Aidha amesema vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi, shule ya msingi Mnyanjani vyenye thamani ya sh milioni 50 ambavyo ni mradi wa uliozinduliwa na mbio hizo mwaka 2023 vitakaguliwa.


"Kutafungualiwa klabu ya wapinga rushwa na dawa za kulevya katika shule hii pamoja na kupokea taarifa ya jinsi halmashauri inavyojiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa 20024" amesema Kaji.

Pia amebainisha mwenge utaweka jiwe la msingi katika zahanati ya Mzingani thamani yake ni sh milioni 150 na kupokea taarifa ya mapambano dhidi ya malaria.

Mwenge wa Uhuru utakagua barabara ya Askari na Lumumba yenye thamani ya sh bilioni 1.2 ikiwa ni ukaguzi wa uendelevu wa miradi iliyowekewa jiwe la msinhi mwaka 2923, lakini pia utafungua barabara ya Jumbe na Dunia Hotel yenye urefu wa km 1.2 yenye thaman ya shilingi milioni 817.

Vilevile utakapokea risala ya utii ya wananchi wa halmashauri ya jiji kwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, na kukagua kongamano la vijana, pamoja na kukagua shuhuli za kijamii katika eneo la mkesha ambako ni uwanja wa shule ya sekondari Usagara.

Hata hivyo Kaji ametoa wito kwa wakazi wote wa Wilaya ya Tanga kujitokeza kwa wingi katika mapokezi, katika njia utakapopita mwenge wa uhuru katima maeneo yavmiradi na eneo la mkesha.


"Mkesha utafanyika katika shule ya sekondari ya Usagara, tumeandaa burudani ya kutosha, Mwenge ni furaja, tunataka hilo lionekane kweli, baada ya shuhuli nzima ya mchana, ikifika jioni wote tukutane pale tufurahi na kukesha na mwenge wet wa uhuru,


'Mwenge wetu mwaka huu umebeba kaulimbiu ya 'Tunza mazingira na Shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu" ameongeza Kaji.

Post a Comment

0 Comments