Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE VITI MAALUMU MKOANI TANGA AIWEZESHA UWT MKOANI HUMO KUENDELEZA SIASA KIUCHUMI.


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

JUMLA ya mifuko ya mbegu za mazao ya aina mbalimbali zenye thamani ya sh. milioni 12.5, zimekabidhiwa kwa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Tanga ikiwa ni harakati za kumuwezesha mwanamke kiuchumi kupiyia kilimo ndani ya chama hicho.

Mbegu hizo zikiwemo alizeti, mahindi, mchicha, nyanya, maharage na ngano zimetolewa kwa wanawake hao wa Wilaya zote za Mkoa huo kulingana na hali ya hewa ya eneo la uzalishaji wa kilimo.

Wakina mama hao walikabidhiwa mbegu hizo katika halfla fupi iliyofanyika wilayani Korogwe ambapo pia misaada mbalimbali ilikabidhiwa katika hospitali ya Wilaya hiyo (Magunga).

Akikabidhi mbegu hizo, Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge amesema lengo la Ccm ni kumuinua mwanamke kiuchumi ndani ya siasa hivyo dhamira yake imemsukumua kutoa mbegu bora ili kuwawezesha wanawake mkoani humo.

"Mwaka jana niligawa mbegu katika Wilaya sita tuu, lakini nilikaa nikafikiria nikaona ni vizuri nikagawa kwa Mkoa mzima ili wanawake wengi wapate kufanikisha kilimo ambacho kitawasaidia hata ndani ya chama kwa matumizi madogo madogo,

"Naomba mnielewe kwamba, dhamira yangu ni kuwa ninyi wanawake wa UWT kujikwamua kiuchumi na kusonga mbele kutoka hapa mlipo na kupiga hatua mbele" amesema Ulenge. amesema.

Aidha Ulenge amewasihi wanawake hao kuonesha dhamira yao ya kutaka kujikwamua kwa kufanya kilimo cha mfano kupitia mbegu hizo huku akiwasisitiza kufuata ushauri wa wataalamu wa kilimo ili kuleta tija

Ulenge pia amewataka Maofisa ugani mkoani humo kuacha tabia ya mazoea ya kukaa maofisini na vijiweni, badala yake kuwafuata na kuwatumikia wanawake hao katika maeneo yao ili iwe wepesi kwao kufanikisha dhamira yao.

"Na ninyi Maofisa ugani nawaomba muwe wepesi kutoa ushirikiano kwa wakina mama hawa katika kilimo chao ili waweze kuleta tija na kujikwamua kiuchumi " amesisistiza Ulenge.

Ulenge amewaeleza wanawake hao kuwa hawataweza kuendelea bila kufanya shughuli za kimaendeleo na kujikwamua kiuchumi, ikiwemo kilimo.

Mwenyekiti wa UWT, Wilaya ya Korogwe mji Sophia Mhina amesema kuwa, kupitia mbegu walizopewa, wataweza kulima zao la alizeti kwa wingi na kufikia hatua ya kupanga vidumu vya mafuta pembezoni mwa barabara kuu ya Arusha - Dar es salaam.

Hata hivyo mwenyekiti wa UWT Korogwe vijijini Hadija Mshahara amebainisha kwamba wanajivunia ukombozi wanaoupata kutoka kwa mbunge huyo kwani anachokifanya inaonesha tosha kuwa anawajali na kuwathamini wanawake wa Mkoa huo.

Akiongea wakati wa ufungaji wa hafla hiyo, mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Korogwe vijijini, Ally Waziri amewataka maofisa ugani kuwasaidia wakina mama hao kwa kuwapa elimu na ushauri juu ya zao hilo huku akiomba kuwepo na utaratibu wa uoteshaji wa mbegu kwa ajili ya kilimo cha baadaye.

"Wataalamu wa kilomo waangalie namna ya kuzalisha mbegu bora ili wakulima wapate unafuu wa kununua mbegu kila mwaka, kutokana na kiluisha kwa ubora wa mbegu kuisha baada ya kupandwa zaidi ya mara mbili" amebainisha.

Post a Comment

0 Comments