Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DK.MWINYI AONGOZA DUA KUMBUKUMBU YA KARUME

-Dk. Mpango, Kinana, Nchimbi, Majaliwa washiriki

Na Mwandishi Wetu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaongoza wananchi na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali katika dua maalumu ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Dua hiyo ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, dini pamoja wananchi imefanyika leo Jumapili Aprili 7, 2024, katika Ofisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kisiwandui, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Hayati Sheikh Karume aliyeuwawa Aprili 7, mwaka 1972.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria dua hiyo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Komredi Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla pamoja na viongozi wengine waandamizi.

Post a Comment

0 Comments