Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali ipo katika hatua za mapitio ya Kanuni za Usimamizi wa Taka ngumu za mwaka 2009 kwa lengo la kuhakikisha wazalishaji wa chupa za plastiki wanawajibika kuhakikisha taka zitokanazo na chupa za plastiki hazizagai kwenye mazingira.
Amesema hayo wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Kutokana na hali hiyo Mhe. Dkt. Jafo ametoa maelekezo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais kuhakikisha wataalam kwa kushirikiana na wadau wanakamilisha kanuni hizo kabla ya mwisho wa Juni 2024 na kusisitiza rasimu ya kwanza iwe imekamilika ifikapo wiki ijayo.
Aidha, ametoa wito kwa wadau kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni ili zipatikane kanuni zitakazosaidia kuondoa changamoto ya kuzagaa ovyo kwa chupa za plastiki katika mazingira yetu.
Uamuzi huo umetokana na majadiliano ya kina kati ya Serikali, wazalishaji wa chupa za plastiki nchini na wadau wa mazingira. Majadiliano hayo yameongzea chachu katika mapitio ya kanuni hizo.
“Imani yangu Watanzanaia wote ujumbe huu utawafikia na haya tuliyojadiliana hapa ni maamuzi yenye maslahi mapana kwa pande zote yaani Serikali na wadau.
“Kutokana na michango mizuri ya wadau, niwahakikishie ndugu zangu tunakwenda kutengeneza kanuni ambazo zinatamfanya kila mzalishaji atambue ya kwamba ukusanyaji wa chupa za plastiki unakuwa ni wa lazima na si hiyari tena na hapo tutakuwa tumeokoa mazingira,“ amesisitiza Dkt. Jafo.
Pindi Kanuni hizo zitakapokamilika, Waziri Jafo ametoa maelekezo kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuzisimamia kikamilifu na kuchukua hatua kwa yeyote ambaye chupa yake itaonekana inazagaa ovyo mitaani.
Pamoja na hayo, amesema kuwa Serikali inatambua dhamira nzuri ya uwekezaji kutoka kwa wadau mbalimbali ambao wanakuza uchumi wa nchi lakini uwekezaji huo uendane na utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bi. Christina Mndeme amesema amepongeza jitihada za Waziri Jafo za kusimamia usafi wa mazingira.
Bi. Mndeme amesema kuwa usafi wa mazingira ni jambo ambalo huvutia watalii ambao wanakuja ahapa nchini na hivyo kuingiza kipato cha nchi.
Nae, Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi amesema kikao ni jitihada za kutafsiri zile R nne za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambazo ni upatanishi, kuvumiliana na kujenga nchi.
Amesema masuala yanayoamualiwan kupitia kikao hicho na wadau wa chupa za plastiki ni ya kujuenga na kuendeleza kufanya biashara huku mazingira yakitunzwa.
”Tutakumbuka mwezi Februari hadi Machi katika Mkutano wa UNEA 6 moja ya ajenda ilikuwa ni suala la chupa za plastiki ambapo ni miongoni mwa mambo ya kimataiga hivyo Mheshimiwa Waziri anatekeleza,” amesema Mitawi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi akizungumza wakati wa kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, wkiwa katika kakao kilichoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo na kufafanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja Wadau mbali mbalimbali mara baada ya kikao na wadau wanaozalisha bidhaa zinazofunganshwa kwenye chupa na vifungashio vya plastiki kwa ajili ya kujadili kwa pamoja mikakati ya usimamizi thabiti wa uchafuzi wa mazingira utokanao na kuzagaa kwa chupa hizo, kilichofanyika jijini Dodoma leo Aprili 17, 2024.
0 Comments