Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT. BURIANI - JITOKEZENI KUWANIA FURSA ZA KIUCHUMI KULETA MAENDELEO


Na Hamida Kamchalla, TANGA 

WANANCHI Mkoa wa Tanga wametakiwa kutopuuzia fursa mbalimbali zinazowafikia kupitia maonesho katika nyanja tofauti badala yake wachangamke na kuziendea ili kujiletea maendeleo yao na Mkoa kwa ujumla.

Wito huo ameutoa mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi, Dkt. Batilda Biriani alipotembelea mabanda ya maonesho katika maadhimisho ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea kufanyika jijini Tanga.

Dkt.Batilda amesema maonesho kama hayo yanapokuwepo kazi yake siyo kuelimisha, kuhabarisha na kuburudisha tu bali pia yanakuza uchumi katika maeneo husika.

"Maonesho haya pamoja na mengine yanapokuwepo mahali huleta uchumi shindani kwakuwa watu wanakwenda kubadilishana uwezo katika kuelimishana na hata Ujuzi" amesema Dkt. Buriani.

Post a Comment

0 Comments