Ticker

6/recent/ticker-posts

FDH YATOA MAFUNZO KOZI YA LUGHA YA ALAMA KWA WAFANYAKAZI SUMAJKT

Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Shirika la Kuhudmia Watu Wenye Ulemavu (FDH) limeanza kutoa mafunzo ya kozi ya lugha ya alama kwa baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) ili kuwasaidia kuwasiliana na kundi hilo muhimu.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa SUMA JKT Luteni Kanali Dora Kawawa alisema mafunzo hayo kwao ni fursa kubwa kwakuwa kupitia kampuni zao wanafanya kazi na watu tofouti tofauti wakiwemo wenye ulemavu wa kusikia.

“Nyinyi mnaoanza kupokea mafunzo haya ni wawakilishi katika shirika ,najua shirika linaandaa utaratibu na mafunzo haya yatakwenda kusambaa katika kanda zote kadri itakavyopangwa,naomba tuchukulie hoo kama fursa yakujua lugha ambayo itatusaidia kuwasiliana na kundi hili maalum ambao ni miongoni mwa wateja zetu hivyo tutawaeza kuwafikia,”alisema Luteni Kanali Kawawa.

Alisema mafunzo hayo yatahusisha jinsi yakuwasiliana kwa alama,yakuwatambua watu wenye ulemavu wa kusikia,kujua nini anataka na namna kumuhumudumia mteja.

Alisema kampuni hiyo inafanya biashara na watu tofauti tofauti hivyo hawana ubaguzi na kwamba lengo lao ni kuwafikia wateja wa aina zote.

Alisema mafunzo hayo ya mwezi mmoja yatatolewa kwa wafanyakazi waliopo jijini Dar es Salaam na kwamba baada ya hapo wahusika watafanya kazi mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa FDH Michael Salali alisema kundi la watu wenye ulemavu ni miongoni mwa makundi yaliyopo katika jamii yana changamito kubwa ikiwemo upatikanaji mdogo wa huduma kutokana na kutoelewana na watoa huduma hasa viziwi na watu wasiioona.

“Umuhimu wa mafunzo utawezesha kuongeza wigo wa mawasiliano na watoa huduma,katika utoaji wa huduma hizi kumekuwa na changamoto hasa kwa wanaohudumoa,baada ya haya hawa tunaowafundishwa watakuwa watoa huduma wazuri kwa kundi hili,”alisema Salali.

Alisema mafunzo yatamfundisha pia namna yakumtambua mtu mwenye ulemavu na jinsi yakuishi naye,baada ya mafunzo haya watapewa vyeti.

Alisema kuanza kwa mafunzo haya ni muendelezo wa programu nyingine ya mafunzo hayo ambapo yatafanyika katika mikoa mbalimbali ambayo yana ofisi za Suma JKT.

Akizungumzia kuhusu shirika hilo Salali alisema taasisi imefanikiwa kufanya kazi nyingi hasa yenye mlengo yakusaidia watu wenye ulemavu.

“Kundi la watu wenye ulemavu ni miongoni mwa makundi yaliyopo katika jamii yana changamito kubwa ikiwemo kupatikanaji mdogo wa huduma kutokana na kutoelewana hasa viziwi na watu wasiioona.

Post a Comment

0 Comments