Ticker

6/recent/ticker-posts

KOLANDOTO YAJA NA HABARI NJEMA KWA WANAOJIUNGA NA HUDUMA ZA AFYA.



Na Hamida Kamchalla, TANGA.

IMEELEZWA kwamba wataalamu wengi wa wanaotaka kujiunga na masomo ya huduma za Afya ngazi ya kati nchini wanashindwa kuendelea kutimiza ndoto zao kutokana na garama kubwa za uendeshaji wa mafunzo hayo.

Kufuatia hali hiyo serikali imeombwa kuwaangalia na kuwasaidia wataalamu hao ambayo Kwa asilimia kubwa wanahitajika katika jamii kutokana na wengi wao kutoka katika familia ambazo hazina uwezo.

Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Shinyangqa Kolandoto, mkoani Shinyanga Paschal Shiluka amebainisha hayo kwenye Maadhimisho Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika jijini Tanga.

"Kama walivyofanya kwenye mafutanzo ya radiolojia, basi wasaidie na mafunzo haya ili wataalamu wengi wanaoshindwa kumudu garama hizi waweze kujiendeleza,

"Hii itasaidia sana hata kupata wataalamu wengi zaidi ambao wanahitajika sana kwenye jamii, lakini pia tutakuwa tumewapunguzia garama wale ambayo hawana uwezo na hatimaye familia zao zitakaa Kwa amani" amesema.

Shiluka amefafanua kuwa msaada wanaotamani serikali ifanye ni kutoka mikopo kwa wataalamu hao wa ngazi ya kati na kwakuwa ndiyo wengi hata Bodi ya Mikopo itanufaika zaidi kuliko hata Kwa walioko katika vyuo vikuu.

"Hawa ndiyo wanaojiriwa kwa wingi, kwahiyo hata wakipatiwa Mikopo kurudisha kwao itakuwa rahisi, takwimu zinatuonesha kwamba wanafunzi wengi wanapenda na wanajiunga lakini wanapofika njiani wanakwana, na hii inatuumiza sana kwa kuona nguvu kazi kubwa inapotea bure" amesema.

Kwa upande wake Ofisa Masoko Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Josephine Charles amesema chuo hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wanaomaliza masomo yao chuoni hapo na kuwapatia fursa za ajira zinazohusu masuala yote ya afya..

"Kwahiyo tunawafundisha wanafunzi Kwa weledi na taaluma lakini pia mwisho wa siku tunawapatia ajira na wanakwenda kwa jamii ambapo zinawajenga na wamekuwa wakifanya vizuri" amesema.

Post a Comment

0 Comments