TAASISI isiyo ya kiserikali ya LALJI FOUNDATION imetoa msaada wa viungo bandia kwa wagonjwa 11 katika hospitali CCBRT Dar es es salaam ikiwa ni sehemu ya malengo ya taasisi hiyo kuendelea kugusa makundi mbalimbali yenye uhitaji katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa taasisi ya LALJI FOUNDATION Katibu wa taasisi hiyo ndugu Fatema Lalji amesema kuwa hii ni mara ya pili taasisi hiyo kukabidhi viungo bandia kwa wagonjwa na kusisitiza kuwa zoezi hilo litakua endelevu ili kuendelea kuwafikia watu wengi zaidi.
Amebainisha kuwa lengo ni kugusa watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii ambapo pia amewataka wadau na watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha viungo bandia CCBRT Dr Ruth Onesmo ameishukuru taasisi hiyo kwa kutoa msaada huo na kutoa wito kwa wadau wingine kua na moyo wa kutoa msaada kwa watu wenye mahitaji maalum.
0 Comments