Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU KATIBU MKUU UJENZI AMPA TANO RAIS SAMIA UKAMILISHAJI MIRADI YA MAENDELEO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Bw Ludovick Nduhiye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza na kukamilisha miradi katika sekta ya ujenzi.

Ametoa shukrani hizo leo tarehe 28 Mei 2024 katika viwanja vya Bunge wakati akifunga maonesho ya siku mbili ya wizara ya Ujenzi Pamoja na taasisi na wakala zake, ambayo yalikuwa na lengo la kuonyesha kazi zilizofanywa na zinazoendelea kufanyika katika sekta ya Ujenzi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Nduhiye amesema kuwa Rais Samia katika kipindi cha miaka mitatu tangu ameingia madarakani amefanikisha kukamilika kwa miradi mikubwa na midogo huku miradi mingine ikiwa inaendelea kwa kasi kubwa.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni Pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba na majengo ya serikali, miundombinu ya Barabara, Madaraja, Viwanja vya ndege na vivuko.

Post a Comment

0 Comments