Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. SAMIA MGENI RASMI MKUTANO WA UVUVI BARANI AFRIKA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wa Uvuvi barani Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024) ambao utafanyika Julai 5-7 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo  unalengo la kuimarisha umoja wa Afrika na kuwasilisha maoni ya Mkutano huo katika mikutano ya kimataifa kama Sauti Moja ya Afrika.

Pia Mkutano huo utajumuisha maadhimisho ya miaka 10 ya utekelezaji wa Mwongozo wa Uvuvi Mdogo na Muundo wa kisera wa kusimamia Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji barani Afrika, lakini pia utaangazia fursa zilizopo katika Uchumi wa Buluu.

Ameyasema hayo leo Mei 23, 2024 Jijini Dar es Salaam, na Waziri wa Mifumo na Uvuvi, Abdallah Ulega wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye Mkutano huo ambao utahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika.

"Mkutano huu utakuwa chachu ya kubadilishana mawazo, fursa na teknolojia mbalimbali za kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa kwenye utekelezaji wa dhana ya kujenga kesho iliyo bora kwa vijana wetu (BBT), na kufikia malengo makubwa kwenye Uchumi wa Buluu."

Amesema pamoja na mambo mengine, mkutano huo utatumika kama Jukwaa litakolokutanisha wavuvi kutoka nchiniTanzania na wenzao kujadili mafanikio na changamoto zinazowakabili dhidi ya mustakabali wao

Aidha Waziri Ulega amesema mkutano huo unatarajia kujumuisha viongozi na wataalam wa sekta ya Uvuvi kutoka Afrika, Wawekezaji na Wafanyabiashara wakubwa barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla, Taasisi zisizo za Kiserikali, Taasisi za Kikanda, Watafiti, Vyuo Vikuu, na Wavuvi Wadogo ambao ndiyo wahusika wakuu wa Mkutano huu.

Waziri Ulega ameyataja manufaa mbalimbali ambayo nchi itayapata kupitia Mkutano huu ikiwa ni pamoja na Kufungua fursa za uwekezaji kwenye sekta ya Uvuvi, Kufungua wigo wa masoko ya nje ya mazao ya Uvuvi ya nchini Tanzania, kuongeza uwanda mpana wa wavuvi nchini kujifunza namna ya kuendesha shughuli zao kisasa ili uvuvi wao uwe na tija, kuendelea kuboresha mahusiano ya matumizi ya rasilimali za maji ya asili na zile za ukuzaji viumbe maji, baina wa wadau  wa Sekta ya Uvuvi  waliopo hapa nchini na wale wa mataifa mengine barani Afrika na Ulimwenguni kwa ujumla.

Mbali na hayo, Waziri Ulega amewakaribisha wadau wote wa Sekta ya Uvuvi waliopo nchini kushiriki katika mkutano huo, na kuhakikisha wanatumia siku zote za Mkutano huo kuongeza tija, kwenye shughuli zao za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe maji.

Waziri wa Mifumo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Mkutano wa Uvuvi barani Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024) ambao utafanyika Julai 5-7 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (uvuvi), Dkt. Edwin Mhede.

Waziri wa Mifumo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Mkutano wa Uvuvi barani Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024) ambao utafanyika Julai 5-7 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mifumo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Mkutano wa Uvuvi barani Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024) ambao utafanyika Julai 5-7 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (uvuvi), Dkt. Edwin Mhede.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (uvuvi), Dkt. Edwin Mhede akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 23, 2024 Jijini Dar es Salaam kuelekea Mkutano wa Uvuvi barani Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024) ambao utafanyika Julai 5-7 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Mifumo na Uvuvi, Abdallah Ulega (hayupo pichani) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 23, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa Mkutano wa Uvuvi barani Afrika (AFRICA SMALL SCALE FISHERIES SUMIT 2024) ambao utafanyika Julai 5-7 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments