Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAGDSS WAIOMBA SERIKALI KUSIMAMIA VIPAUMBELE VYOTE VYA BAJETI HUSIKA

WADAU wa Semina za Jinsia na Maendeleo ( GDSS), wameiomba Serikali kusimamia na kufuatilia vipaumbele vyote vinavyoachwa katika bajeti na kuhakikisha vinafanyiwa kazi ipasavyo ili kuondoa chagamoto mbalimbali zinazokabili wananchi.

Ombi Hilo limetolewa Mei 29,2024 Jijini Dar es Salaam na washiriki wa semina hizo ambazo zinafanyika kila Jumatano katika ofisi za TGNP-Mtandao walipokuwa wakijadiri bajeti ya Wizara ya Afya 2024/2025.

Wanaharakati hao walisema kuwa wamebaini bajeti ya Wizara ya afya iliyowasilishwa hivi karibuni na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu haijagusa makundi yote ingawa bado kuna makundi yanaitaji msaada na hayajakuishwa moja kwa moja.

"Bajeti ya Wizara ya afya iliyowasilishwa hivi karibuni haijagusa kwa vitendo bali imegusa kwa maeneo tu tunaomba Serikali isimamie vyema vipaumbele vinavyokuwa vinaainishwa katika bajeti hii itasaidia kuondoa chagamoto mbalimbali katika jamii pia tunaomba ifatilie matamko ambayo yamekuwa yakitolewa"walisema

Akizungumza katika semina hiyo Mwanaharakati ngazi ya jamii Bi.Aisha Msuli alisema kuwa bado wajawazito, wazee chini ya umri wa miaka 60 na watoto chini ya miaka mitano awapati huduma bure pindi wanapokwenda hospitali.

"Mama mjamzito anapofika hospitali bado amekuwa akitakiwa kutoa fedha Kwa ajili ya kupata kadi ya kiliniki licha ya Serikali kusema kuwa ni bure"Bi.Aisha alisema

Naye,Mdau Mdau wa masuala ya Jinsia Bi.Maua Kilima alieleza kuwa licha ya kuwepo kwa masanduku ya kutoa maoni katika baadhi ya hospital lakini maoni hayo yamekuwa hayafatiliwi ipasavyo.

ambapo aliiomba Serikali kufatilia kwa karibu maoni hayo ili kuweza kutatua chagamoto wanazokumbana nazo wananchi pindi wanapofika hospitali.

Kwa upande wake,Mwanaharakati wa wa Jinsia Mwafaraja Selasela aliiomba Serikali kuongeza vituo vya afya na kuhakikisha vinaendana na hadhi ya huduma zinazotolewa.

"Mazingira bado ni chagamoto katika baadhi ya vituo vya afya .. pia wataalamu nao awatoshelezi hivyo naiomba Serikali iliangalie suala hili Kwa ukaribu"alisema

Pia alisema kiwango cha dawa kinachotolewa ni kidogo zaidi na kimekuwa kikipelekea wagonjwa kukosa dawa pindi wanapoenda hospitali na kuishia kupewa panado

Denis Victoria alisema ni muhimu Serikali itoe we bei elekezi ya dawa ili kuondoa sitofahamu kwao.

"Unaweza kwenda katika duka fulani la dawa unakuta dawa inauzwa bei tofauti tofauti hivyo naomba Serikali iweke bei elekezi ili kuondoa chagamoto hiyo.

Naye mdau aliyeshiriki katika semina hiyo Ayoub Sharif aliiomba Serikali kuhakikisha huduma ya pedi inapatikana bure mashuleni kwani ni huduma kama huduma nyingine.

Emmanuel Jigumi aliiomba jamii kufuatilia na kushinikiza viongozi husika ili kuweza kuwepo Kwa ufatiliaji masuala yote yanayotolewa.

Aidha amesema ni muhimu jamii kuchagia viongozi watakaoweza kusimamia wananchi vizuri

Post a Comment

0 Comments