Ticker

6/recent/ticker-posts

WASANII WA FILAMU WAMVULIA KOFIA RAIS SAMIA,STIVE NYERERE AMTAJA NI MKOMBOZI WAO


WASANII wa Sekta ya Filamu Nchini wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa heshima kubwa ya kuifanya sekta hiyo kuwa ya Kimataifa.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa kauli ya hivi karibuni ya kuanza kusafiri na wasanii nje ya nchi akiwa katika Uzinduzi wa Albam ya Harmonize 'Muziki wa Samia'

Wakitoa pongezi hizo Jijini leo mapema jiji Dar es salaam wamesema jambo hilo ni kubwa linakwenda kutagaza tasnia ya Filamu.

Akizungumza na waandishi wa habari Kwa niaba ya wasanii hao Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steve Nyerere amesema kauli iliyotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imewaunganisha wasanii wa Filamu na imelenga kuwainua kiuchumi.

"Tunamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametupa heshima kubwa na ametuheshumisha ...Rais wetu alipotoa tamko hili asilimia kubwa ya wasanii wa filamu awakulala "amesema

Hata hivyo,stive amewaomba watakaoteuliwa kuongozana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuitumia fursa hiyo vizuri ikiwa ni pamoja na kutagaza utamaduni wa kitanzania.

Kwa upande wake Msanii Chuchu Hans amemshukuru mama kwa nafasi nzuri aliyowapatia imewapa nguvu sana.

Naye Suzan Natasha mwingizaji amesema tamko la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imeweka historia kwa wasanii wa filamu kwani limenyanyua vitu vipya katika moyo Yao.

" Tunashukuru sana mama Tunakupenda na tupo na wewe tunamshukuru Mungu tutaendelea kukuunga mkono katika hatua mbalimbali"amesema

Naye Msemaji wa Chama cha Waigizaji Jimmy Mafufu amebainisha kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amegundua kuwa tasnia ya Filamu ni jamii ya kuambatana nayo.

Post a Comment

0 Comments