Ticker

6/recent/ticker-posts

AJALI ZA BODABODA BADO CHANGAMOTO NCHINI

MENEJA wa utafiti kutoka taasisi ya mifuoa MOI Dkt Joel Bwemelo amesema taasisi hiyo hupokea majeruhi wa ajali 8000 Kwa mwaka na asilimia 40 ya majeruhi hao wanatokana na ajali za pikipiki zinazobeba abiria maarufu kama Bodaboda.

Ni katika hafla ya utiaji Saini hati ya makubaliano baina ya chuo Cha taifa Cha usafirishaji na taasisi ya mifuoa MOI ambayo pamoja na mambo mengine yatasaidia kuweka mikakati ya pamoja ya kubadilishana ujuzi ili Kwa lengo la kupumguza ajali za barabara.

Meneja Utafiti MOI Dkt Joel Bwemelo amesema licha ya jitihada zinazofanyaa na serikali Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lakini Bado idadi ya majeruhi wanapelekewa kwenye taasisi hiyo Bado inazidi kuongezeka.

Baadhi ya waendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodabida jijini Dar es salaam wamekuwa na maoni tofauti kuhusu ajali hizo wengine wakitumia lawama madereva wa magari kiwasababishia ajali

Wakati huohuo chuo Cha taifa Cha usafirishaji NIT na Kampuni ya usafirishaji ya SSCS zimehuisha makubaliano ya Kwa miaka mitatu mingine ambayo pamoja na mambo mengine kampuni huyu itakuwa ikipokea wanafunzi kutoka NIT Kwaajili ya kuwapatia mafunzo ya ujuzi wa kazi

Msisitizo Kwa madereva wa vyombo vya moto ni kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kutokomeza kabisa ajali ya barabarani

Post a Comment

0 Comments