Ticker

6/recent/ticker-posts

BRELA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUWEKA ULINZI MAJINA YAO YA BIASHARA KWA KUYASAJILI

NA EMMANUEL MBATILO, MOROGORO

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamewataka wafanyabiashara kusajili majina ya biashara zao ili kuweza kupata ulinzi wa kisheria na mtu mwingine asiweze kutumia jina lako katika uendeshaji wa biashara.

Ameyasema hayo Juni 19,2024 Mkoani Morogoro na Mkuu wa Sehemu ya Kampuni kutoka Kurugenzi ya Kampuni na Majina ya Biashara wa BRELA Lameck Nyange wakati akiwasilisha mada iliyohusu majina ya biashara na umuhimu wa kusajili katika Mafunzo ya Siku nne ya BRELA kwa Waandishi wa habari wanaoripoti Mkoa wa Dar es Salaam

Akifafanua zaidi amesema watu wanafanyabiashara kwa kutumia majina yasiyosajiliwa na hivyo hawana ulinzi wa kulindwa.“Anayepewa ulinzi ni yule ambaye amesajili. Mtu anaweza kuja kusajili jina lake na wala halifanyii kazi na sheria haijatoa mamlaka ya kufuatilia kwanini aliyesajili jina la biashara halifanyii kazi

“Ili kupata ulinzi wa kisheria unapaswa kuwa umesajili jina lako la biashara na mtu mwingine akalitumia unaweza kumshitaki mahakamani.Hivyo faida mojawapo ya kusajili jina la biashara ni kupata haki ya kumshitaki aliyetumia jina lako.”

Aidha amesema Kuhusu faida za kusajili jina la biashara mbali ya kuwa umeliweka katika ulinzi, pia inasaidia mhusika kupata fursa mbalimbali zikiwemo za kifedha kama kupata mkopo lakini faida nyingine mtu anakuwa amefanya biashara muda mrefu na amekuwa maarufu lakini kwasababu hujasajili mtu mwingine anasajili, hivyo ukisajili hakuna anayeweza kusajili tena.

Post a Comment

0 Comments