Ticker

6/recent/ticker-posts

CCWWT WATOA TAMKO KUPINGA UKATILI KWA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINO).


Na Hamida Kamchalla.

CHAMA cha Wazee Tanzania (CCWWT) kinaungana na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa salamu za rambarambi kwa familia ya mtoto marehemu Asimwe Novato mwenye Ulemavu wa ualbino aliyeuwawa kikatili.

Kiongozi mkuu wa CCWWT Tadey Mchena ametoa salamu kwa familia hiyo kufuatia ukatili uliofanywa kwa mtoto wao aliyeuwawa na kisha mwili wake kutekeleza na watu wasiojulikana katika kijiji cha Gulamula, wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera.

Mchena amesema mbali na salamu hizo CCWWT kinapinga vikali vitendo vya kikatili vinavyotekelezwa na watu wasio na huruma wala hofu ya Mungu.

"Kitendo hiki cha kikatili hakikibaliki katika nchi yetu, kila mtu ana haki ya kuishi, kama CCWWT tumesikitushwa sana na kitendo hiki, tunaomba uchunguzi ufanyike haraka na ikibainika watuhumiwa wachukuliwe hatua za kisheria ili iwefundisho kwa wote wenye tabia za kupenda kukatusha maisha ya wengine,

"CCWWT tunategemea kuanza ziara rasmi ya kuzunguuka Wilaya zote 189 nchini kupinga ukatili kwa watoto, wenye ulemavu lakini pia ukatili kwa wazee, lakini pia tunalenga kuandikisha wanachama wapya nchini kote ikiwa ni pamoja na kujenga na kuimarisha chama chetu" amesema Mchena.

Pichani : Kiongozi mkuu wa Chama Cha Wanaume Wazee nchini (CCWWT), Tadey Mchena.

Post a Comment

0 Comments