Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA ATEMBELEA KITUO CHA KUBADILISHANA MAARIFA YA KIDUNIA NA MAENDELEO (GKED) KILICHOPO SEOUL KATIKA NCHI YA JAMHURI YA KOREA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Korea Dkt. Dong Soo Kang wakati wakimsikiliza Mtafiti wa Kituo cha Kubadilishana Maarifa ya Kidunia na Maendeleo (GKED) Hyerin Byun kuhusu Mafanikio mbalimbali ya Teknolojia ya Kisasa katika Kituo hicho kilichopo Seoul, Jamhuri ya Korea tarehe 01 Juni, 2024.
.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtafiti wa Kituo cha Kubadilishana Maarifa ya Kidunia na Maendeleo (GKED)Hyerin Byun kuhusu safari ya Mafanikio ya Nchi ya Jamhuri ya Korea wakati alipotembelea Kituo hicho kilichopo Seoul nchini humo tarehe 01 Juni, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya video fupi kuhusu Teknolojia ya Kisasa wakati alipotembelea Kituo cha Kubadilishana Maarifa ya Kidunia na Maendeleo (GKED) kilichopo Seoul katika nchi ya Jamhuri ya Korea tarehe 01 Juni, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Korea Dkt. Dong Soo Kang wakati wakitazama video fupi kuhusu safari ya maendeleo ya nchi ya Jamhuri ya Korea mara baada ya kuwasili katika Kituo cha Kubadilishana Maarifa ya Kidunia na Maendeleo (GKED) kilichopo Jijini Seoul tarehe 01 Juni, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Korea Dkt. Dong Soo Kang katika picha na Mawaziri alioambatana nao pamoja na Balozi wa Tanzania katika Nchi ya Jamhuri ya Korea Mhe. Togolani Mavura mara baada ya kutembelea Kituo cha Kubadilishana Maarifa ya Kidunia na Maendeleo (GKED) kilichopo Jijini Seoul tarehe 01 Juni, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Korea Dkt. Dong Soo Kang mara baada ya kutembelea Kituo cha Kubadilishana Maarifa ya Kidunia na Maendeleo (GKED) kilichopo Jijini Seoul tarehe 01 Juni, 2024


.

Baadhi ya Televisheni, Typewriter na Simu za mezani zilizotumika zamani katika Nchi ya Jamhuri ya Korea zikiwa zimehifadhiwa kwenye Kituo Kubadilishana Maarifa ya Kidunia na Maendeleo (GKED) kilichopo Jijini Seoul tarehe 01 Juni, 2024.

Post a Comment

0 Comments