Ticker

6/recent/ticker-posts

WALIOLAWITI NA KUBAKA WATOTO WILAYANI HANDENI, RC TANGA ATOA MANENO MAZITO


NA Hamida Kamchala, HANDENI.

WATOTO wapatao nane wamebakwa na kulawitiwa baada ya kurubuniwa kwenye kibanda cha kukaangia mihogo kilichopo karibu na shule yao katika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga.

Mkuu wa Mkoa Tanga Balozi Dkt Batilda Burian amelsikittishwa na kulaani vikali kitendo hicho na kuagiza kufanyika kwa kura za siri ili kubaini watu wote wanaouhusika lakini pia kuunga mkono vitendo hivyo wilayani humo.

Balozi Dkt Burian amesema kitendo cha aina hiyo pia kimeripotiwa katika Wilaya ya Mkinga ambapo alizitaka jamii kujipanga na kupambana vikali na vitendo hivyo ambavyo vikiachwa vinaweza kuathiri viazazi vya sasa na vijacho.

Dkt. Buriani ametoa maagizo hayo akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Mji Mkoani Tanga wakati wa baraza maalumu la madiwani la kupokea taarifa za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambapo Halmashauri hizo zilipata hati safi.

Balozi Dkt Burian amesema kuwa iwapo uchunguzi utafanyika na akapatikana mtu yeyote awe mwalimu au kiongozi wa dini yeyote hawatamuacha mtu kwani vitendo hivyo vimekuwa vikidhoofisha nguvu kazi ya Taifa.

"Watoto wadogo nane wamebakwa na kulawitiwa, watu wazima wameanzisha kigenge kumbe kile kigenge ni cha makusudi cha danganya toto, wana shughuli zao nyingine watoto wakienda wanadanganywa na mihogo ya kukaanga,

"Matokeo yake wanaenda wanawadhulumu watoto wadogo wa kike kuanzia miaka 8, 9 mpaka 10, mtoto wa mwisho kubakwa alipata changamoto ya kutokwa na damu nyingi kwa kuwa alikuwa ni mdogo ndio watu wakajua, "amesema Balozi Dkt Burian.

"Nauliza jamani Handeni hili suala halijawachukiza mmekaa kimya nilifikiri mtaenda pale kwa hasira mkiwa mmefunga vibwebwe watoto wamefanyiwa ukatili au mnataka watu wa Mwanza ndio waje na vibwebwe na maandamano kuwasemea nyinyi watu wa Handeni?,

"Sisi tunakiona ni kitu poa na sio kwenu tu Handeni, hata Wilaya ya Mkinga pia nimekuta taba hii, mtoto wa miaka mitatu wa kike amebakwa na kulawitiwa, hivi huyo mtoto amekosa nini na ana dhambi gani? amehoji Dkt. Buriani.

Aidha ameahidi kushuhulikia na kupambana na vitendo hivyo na kuhakikisha sheria inasimama kuchukua hatua iali zinazowastahili watuhumiwa walihusika.

"Kwa kweli mimi nimesema hili jambo tutahangaika nalo na hawa watu tutahangaika nao na wanasheria wanaisimamia hiyo kesi lazima hukumu ipatikane na iwe fundisho na tutaanza kura za siri kutaja walawiti, wabakaji wa watoto wa kike na wakiume,

"Huko mashuleni ipite kura ya siri na wataalamu wanajua nani anaonewa kwa hila na anayefanya kweli, tushirikiane tukikaa kimya hata sisi tutakuwa hatujawatendea haki wanahandeni, "amesisitiza.

"Niwaombe sana sana hili jambo lituume na tulichukie sana hata iwe ni baba mzazi, iwe ni mlezi, kaka au mjomba tulichukie hilo jambo mjmi nasema kuna watu wana agenda yao mataifa ya nje wameshahalisha hilo jambo kwao wanajaribu sasa kutafuta kwa njia ya nyuma kuwafundisha watu na kuwalipa wakiwa wanalenga kizazi kijacho, "amesema Balozi Burian.

Aidha Balozi Dkt Batilda amefafanua kwamba endapo mtoto ataingiliwa kinyume na maumbile atakuwa amepoteza sifa ya kujiunga na majeshi yote nchini jambo ambalo linapaswa kupigwa vita ili kuweza kupata makomando watakaokwenda kupigana maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Sambamba na hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni Mji Mussa Mkombati amekiri kweli kuwepo kwa suala hilo na kueleza kuwa suala hilo wanalishughulikia ipasavyo hadi kufikia kutoa ahadi ya zawadi kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa mtu anayehusika na ubakaji na ulawiti.

"Tunapofanikiwa kumkamata mbakaji au mlawiti tunakosa ushirikiano kutoka kwa jamii kwa maana suala likishakuwa polisi na kutakiwa kwenda mahakamani jamii husika wanalitoa suala hilo nje ya sheria na kulipeleka nyumbani jambo ambalo linatukwamisha katik mapambano yetu, "amesisitiza.

"Bado hatujakata tamaa tunaendelea kupambana kuhakikisha waliohusika na matukio haya sheria inachukua mkondo wake na wanapata adhabu stahiki ikiwa ni pamoja na kuendelea kupambana na wabakaji na walawiti kwa kujnda kamati za kuchunguza wanaotekeleza vitendo hivyo nje na ndani katika shule zote za wilaya hiyo, "amesema Mkombati.

Tukio la wanafunzi wanane kubakwa na kulawitiwa Wilayani Handeni Mkoani Tanga lilifanyika mwanzoni mwa mwezi june mwaka huu ambapo walibaini matendo hayo baada ya binti wa miaka 8 aliyebakwa kwa mara ya mwisho kupata changamoto ya damu na kuwataja wenzake waliokuwa wakifanyiwa vitendo hivyo.

Post a Comment

0 Comments