Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA M. 379 KUBORESHA SHULE ZA MSINGI 5 TANGA JIJI, MRADI WA BOOST.

Ofisa Elimu Halmashauri jiji la Tanga, Mwalimu Shomari Bane akiongea na waandishi wa habari.
Wananchi wa kata ya Mwakidila wakifuatilia mkutano.
Mwalimu Bane akiongea na wananchi wa kata ya Mwakidila.

Na Hamida Kamchala, TANGA.

SERIKALI kupitia Mradi wa BOOST katika kuboresha elimu ya msingi na awali imetoa kiasi cha sh milioni 379.5 kwa halmashauri ya jiji la Tanga kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule tano za msingi jijini humo.

Ofisa Elimu wa Halmashauri ya jiji la Tanga, Mwalimu Shomari Bane aliyasema hayo wakati akiutambulisha mradi huo kwa wakazi wa kata ya Mwakidila, ambapo shule ya msingi Mwakidila ni moja kati ya shule zinazotekelezwa na mradi.

Mwalimu Bane amezitaja shule ambazo zinafanikiwa kupata mradi huo kuwa ni shule ya msingi Kasera ikiwa pamoja na shule shikizi Kasera ambayo imepata kiasi cha sh milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na sh milioni 12.6 kujenga matundu sita ya vyoo,

Mwalimu huyo amesema shule ya msingi Mwakidila pia imepatiwa sh milioni 69.1 kujenga madarasa mawili ya mfano yanayoongea pamoja na matundu 6 ya vyoo, kwa maana ya matundu matatu ya wavulana na matatu ya wasichana.

"Lakini kama haitoshi nimewaomba sana wananchi kutumia nguvu zao kujitolea na michango yao kwa ajili ya kujenga ofisi ya walimu kwa sababu kuna watoto hawa wadogo wa elimu ya awali, hivyo wanapokuwa na ofisi jirani na walimu wao itapendeza zaidi kiusalama" amesema.

Hata hivyo amefafanua kwamba shule za msinui Majengo na Shaban Robbert kila moja zilipatiwa sh milioni 75 kwa ujenzi wa madaeasa matatu pamoja sh milionu 12.6 kwa ajili ya matundu 6 ya vyoo, ambazo zimetenguliwa.

"Lakini kutokana na sababu za uwepo wa uhitaji mkubwa wa baadhi ya shule, fedha zilipangwa kwa ajili ya shule za Majengo na Shaban Robbert zimepekwa kwenye shule zingine za msingi Ziwani na Kange,

"Mradi huu unatekelezwa ndani ya miaka sita, kuanzia mwaka 2021 hadi 2027 na mradi hu tunaukabidhi kwa uongozi wa kata katika shule husika kwakuwa wao ndiyo watakaosimamia mradi huu" amefafanua Bane.

Baadhi ya wananchi wameelezea furaha yao kufuatia mradi navkusema itawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kuweza kukaa madarasanu kwa nafasi kwani vyumba vya madarasa ju vichache ikilinganishwa na wanafunzi waliopo.

Mwenyrkiti wa mtaa wa Mwakidila B, Athumaji Mbulinyingi amesema mradi huo kwa upande wao ni kama upendeleo mkubwa wanaishukuru sana serikali ya awamu ya sita kwani kil9 chao kikubwailikuwa ni kero kubwa sana kwakuwa watoto walikuwa na msongamano mkubwa.

"Tunaishukutu sana serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa upendeleo huu, tuna imani kubwa sana na mradi huu na mimi kama mwenyekiti wa mtaa nitausimamia nikishirikiana na wananchi wangu, nina imani utafanyika na hakutakuwa na dosari yoyote na utafikia hatma pasi na malumbano wala mgogoro wa aina yoyote" amesema.

Post a Comment

0 Comments