Ticker

6/recent/ticker-posts

HAZINA HUTOA PENSHENI KWA WASTAAFU WASIOCHANGIA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Na. Peter Haule, WF, Dar es Salaam

Ofisi ya Pensheni ya Hazina iliyo chini ya Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali inajukumu la kulipa mafao ya kustaafu kwa viongozi wa kitaifa na kisiasa na watumishi wa umma ambao hawachangii katika mfuko wowote wa hifadhi ya jamii.

Hayo yamebainishwa na Afisa Hesabu Mkuu kutoka Kitengo cha Pensheni Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky, wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

Bi. Chacky alisema kuwa aina ya mafao ambayo hutolewa na Hazina kwa mstaafu ni pamoja na kiinua mgongo kwa mtumishi anapostaafu kwa mujibu wa Sheria akiwa na miaka 60 au akistaafu kwa hiari akiwa na miaka kuanzia 55.

Alisema aina nyingine ya mafao ni pensheni ya kila mwezi anayolipwa mstaafu baada ya kustaafu kwa mujibu wa Sheria Sura 371 ya mwaka 1956 na Sheria Na. 2 ya mwaka 2018 ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma.

Bi. Chacky alitaja mafao mengine yanayolipwa na Kitengo hicho kuwa ni pamoja na Mafao ya Mirathi, Pensheni ya kifo, mafao kwa wategemezi, kiinua mgongo kinachotokana na ajali kazini, pensheni ya ulemavu na mafao ya mkataba.

Aidha aliwataka wananchi kutembelea Banda la Wizara ya Fedha ili kupata elimu kuhusu Pesheni inayolipwa na Hazina ili kupata uelewa na pia kuepukana na taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kupotosha.

Afisa Hesabu Mkuu kutoka Kitengo cha Pensheni Wizara ya Fedha, Bi. Joyce Chacky (katikati), akitoa maelezo kwa Mstaafu Mzee Rashidi Mbwego, kuhusu aina ya mafao yanayolipwa na Hazina, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katıka Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Kumbukumbu wa Kitengo hicho, Bi. Neema Nyipamato.

Afisa Kumbukumbu wa Kitengo cha Pensheni Wizara ya Fedha, Bi. Neema Nyipamato, akitoa maelezo ya majukumu ya Ofisi ya Pensheni-Hazina kwa Dkt. Lazaro Mhoja, kuwa ni pamoja na kulipa mafao kwa viongozi wa kitaifa na kisiasa na watumishi wa umma ambao hawachangii katika mifuko ya hifadhi ya jamii, wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Afisa Kumbukumbu wa Kitengo cha Pensheni Wizara ya Fedha, Bi. Neema Nyipamato akitoa maelezo ya majukumu ya Ofisi ya Pensheni-Hazina, kwa Mzee Yahya Faraji, kuwa ni pamoja na kulipa mafao kwa viongozi wa kitaifa na kisiasa na watumishi wa umma ambao hawachangii katika mifuko ya hifadhi ya jamii, wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. Fronto Furaha, akieleza kuhusu umuhimu wa Sera ya fedha katika maendeleo ya wananchi kwa Mzee Adam Zuku, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024.

Afisa Elimu Mwandamizi wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), George Ngelime, akitoa elimu kuhusu Bodi hiyo inavyofanyakazi kwa vijana waliotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2024, ambapo amewapongeza watoa huduma kwa umahiri wao katika kutoa elimu kwa umma.

Mkuu wa Kitengo cha Maktaba Wizara ya Fedha, Bi. Upendo Kavalambi, akieleza umuhimu wa maktaba ya Wizara ya Fedha ambayo inatoa fursa ya kupata taarifa muhimu ya masuala ya fedha na mengine, kwa wakazi wa jijini Dar es Salaam, Bi. Christin Wanyonya na Happy Muhango, walipotembelea Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es Salaam.

Wananchi waliojitokeza kwa wingi katika Banda la Wizara ya Fedha, wakiendelea kupata huduma mbalimbali katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Post a Comment

0 Comments