Ticker

6/recent/ticker-posts

MAFUNDI KIGAMBONI WAPONGEZA UBORA WA RANGI NA WALL PUTTY YA KIBOKO

 


PICHA YA PAMOJA : Baadhi ya Mafundi kutoka Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya Utengenezaji , Uuzaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ujenzi nchini ya KIBOKO PAINTS ambapo kampuni hiyo imetambulisha bidhaa yake mpya ya KIBOKO WALL PUTTY yenye ubora wa hali ya juu kwa mafundi hawa , Mapema leo Julai , 06 , 2024 Katika Ukumbi wa Arena - Kigamboni .Mmoja wa mafundi akiijaribu kwa kuipaka ubaoni KIBOKO WALL PUTTY mbele ya mafundi wenzake , haikuishia hapo WALL PUTTY ya makampuni mengine na yenyewe ilipakwa ili kulinganisha ubora , baada ya kukauka mafundi wamekiri kwamba KIBOKO WALL PUTTY ni bora sana kuliko WALL PUTTY nyingine zote sokoni.
Bwn. Hamidu Satara Afisa Mauzo KIBOKO PAINTS na Modest Jeronimo Meneja Mauzo KIBOKO PAINTS Dar Es Salaam ( waliosimama ) wakipokea na kujibu maswali kutoka kwa mafundi .

 Na Adery Masta. 

Kampuni namba moja nchini kwa uuzaji wa Vifaa mbalimbali vya Ujenzi kama vile Mabati , Rangi n.k  KIBOKO Paints, Imetambulisha Bidhaa yake mpya sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu kwa baadhi ya Mafundi Rangi wanaoishi na kufanya kazi Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam.

 Leo , Julai 6, 2024 akizungumza baada ya Semina hiyo , Bwn. Hamidu Satara ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni, lakini pia Mkufunzi wa Semina hiyo amesema 

" Kampuni ya KIBOKO PAINTS inafanya Semina hizi nchi nzima ambapo kwa upande wa Dar Es Salaam zimeshafanyika Gongo la Mboto na maeneo yake ya karibu , Buguruni na maeneo yake ya karibu , Mbezi , Kariakoo , Mbagala na leo tunahitimisha na Kigamboni kwa awamu hii ya kwanza kwa upande wa Dar Es Salaam na kuanzia wiki ijayo tutakua Morogoro "

" Tunaendelea na Semina hii kwa Mafundi huku tukitambulisha Bidhaa yetu Bora kabisa sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY ambayo imepokelewa na kupendwa na Mafundi kutokana na Ubora wake , KIBOKO WALL PUTTY inaweza kutumika Nje , Ndani , Kufungia Mikanda na Dari , ni nyeupe na inaweza kufanya ukuta wako kung'ara hata kama haujapigwa rangi. "  amesema Bw. Hamidu

                             

Sambamba na hilo , Mafundi wamepata nafasi ya kujionea maboresho makubwa ambayo kampuni ya Kiboko imeyafanya katika rangi zake , ambazo kwa sasa ni bora ukilinganisha na zilivyokua miaka kadhaa iliyopita , mafundi wamepata nafasi ya kuilinganisha rangi ya KIBOKO na Rangi za makampuni mengine kwa kuipiga kwenye ubao ambapo matokea yaliyopatikana baada ya muda mfupi yameonesha dhairi kwamba rangi ya KIBOKO imeboreshwa kwa kiwango kikubwa .

Bwn . Salim Chembe  ni fundi rangi aliyezungumza na Mwandishi Wetu Baada ya Semina hiyo ameipongeza kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa kuileta sokoni KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu , aidha amewapongeza pia kwa maboresho makubwa katika rangi zao

"KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni, lakini pia rangi yao ni nzuri sana  " amesema.

                                      

.

Post a Comment

0 Comments