Ticker

6/recent/ticker-posts

MHE. MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU MAONESHO YA SABASABA

*Apongeza huduma zinazotolewa na Ofisi hiyo pamoja na Taasisi zake

Na, Mwandishi Wetu - Dar Es Salaam

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda ametembelea banda la ushirikiano linalotumiwa kwa pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zilizopo chini yake katika maonesho ya 48 ya biashara ya kimataifa ili kujionea jinsi watumishi wa ofisi hiyo wanavyotoa huduma kwa wananchi na wadau kwa ujumla.

Akiwa katika banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Pinda amepongeza huduma bora zinazotolewa na ofisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi zake.

Kwa upande mwengine, amehimiza wanachi wajitokeze kwa wingi katika maonesho hayo na kutembelea banda hilo ili kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na ofisi hiyo.

Maonesho hayo ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania: Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji,”.

Post a Comment

0 Comments