Ticker

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA NACTEVIT ATEMBELEA BANDA LA VETA SABASABA

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi Tanzania ( Nactevit), Bernadetha Ndunguru amesema bado kuna changamoto ya wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalumu kushindwa kuwaleta shuleni na chuo kupata elimu kwa sababu ni haki yao ya msingi. 

Hayo ameyabainisha na leo Julai, 5 2024 na Mwenyekiti huyo alipotembelea banda la Mamlaka ya na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) lilopo kwenye maonesho ya 48 ya Kibashara ya Kimataifa (DIT). 

"Ni kweli kuna baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto ndani wenye mahitaji maalumu hivyo wanapaswa kuto waficha ndani badala yake waweze kuwaleta VETA wajekujifunza ufundi mbalimbali kama tulivyoshudia kwenye mabanda yao wanafanyakazi na waweze kujiajiri,"amesema Ndunguru.

Amesema kuwa wenye mahitaji maalumu wanapata stadi, ujuzi waweza kujitegemea wao wenyewe.

Ndunguru amesema ametembelea mabanda mbalimbali ameona watu wenye ulemavu wanafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kushona nguo na baadhi ya watu wameka oda za nguo zinatoka vizuri. 

" wengine wanatenageneza mabegi ya shule ya kwenda shule na watu wengeni wanaweza kutumia mabegi hayo chuo cha VETA kinasaidia vijana kuweza kujiajiri kupitia mafunzo waliopata,"amesema 

Ameeleza kuwa VETA wanapotoa mafunzo wasiaangaliea watanzania wa kawaida waangalie na wenye mahitaji maalumu kwasababu na wao wana mahitaji muhimu.

Amesema hicho ni kitu cha pekee kinafanywa na VETA wanaona watu wenye mahitaji maalumu wanavyoshughulika na kazi.

Amesema wakipatiwa ujuzi wa kutosha wateweza kujiajiri ili waweze kuendesha maisha yao ya kila siku.

Post a Comment

0 Comments