Ticker

6/recent/ticker-posts

UDSM YAZINDUA KAMATI KUUBORESHA MRADI WA HEET

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam, kupitia Mradi wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), kimezindua Kamati ambazo zinafanya kazi kwenye maeneo ambayo wanafanya ujenzi ili kuwafikia wadau mbalimbali ambao watatoa maoni ambayo yatasaidia uboreshaji wa mradi wa (HEET).

Akizungumza na wandishi wa habari leo Julai 1,2024 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Mtaalamu wa Masuala ya Usalama wa Mradi Dkt. Edmund Mabuye amesema wametoa mafunzo maalumu kwa kamati hizo sambamba na kuzirasimisha ili zianze kazi rasmi.

Aidha Dkt. Mabuye amesema kamati hizo zinafanya kazi kwa kuhusianisha vipengele mbalimbali ambavyo vinavyohusu usalama wa mradi kwa lengo la kuulinda.

"Maoni yanaweza kutolewa kwenye masuala yanayohusu jamii,yanayohusu Jinsia au yanayohusu masuala ya mazingira ambapo ni kamati moja inafanya kazi kwa kuzingatia vipengele mbalimbali vinavyohusu usalama wa mradi"Dkt.Mabuye amesema.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaaluma za Jinsia,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Lulu Mahaya amesema katika eneo la mahitaji maalumu kuna kipengele cha "Kaseme"ambacho kimejikita katika kupambana na unyanyasaji wa kijinsia hasa wa kingono.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa lengo lao hasa ni kuzuia malalamiko kuwa kesi ambapo wamelenga kusimamia haki ili kuulinda mradi huo usisimamishwe kutokana na kufanyiwa ukatili kwenye maeneo ya ujenzi.

Mradi wa HEET unatarajiwa kufanyika kwa miaka mitano kupitia ufadhiri wa Benki ya Dunia,ambapo umekusudia kukuza elimu ya juu kama chachu ya uchumi mpya wa Tanzania,na kufufua na kupanua uwezo wa vyuo vikuu kuchangia katika maeneo muhimu ya uvumbuzi, maendeleo ya kiuchumi, na umuhimu wa soko la ajira.

Post a Comment

0 Comments