MAMLAKA ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) imeanza kufanya kazi kwa mujibu wa sheria mpya ya manunuzi, ambapo pamoja na mambo mengine inaelekeza zabuni zote za Shilingi bilioni 50 na chini ya hapo zitolewe kwa wazawa.
Mkurugenzi wa Utafiti, Maendeleo, na Ubunifu wa PPRA, Mhandisi Masunya Nashon, ameyasema hayo kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa 48 ya Dar es Salaam na kuelezea kuwa kuanzia Oktoba 1, 2023, sheria mpya ya manunuzi namba 10 ya mwaka 2023 na vifungu vyake kwa mujibu wa tangazo la serikali namba 518 la Juni 2024, ilianza kutumika jambo ambalo limeongeza wigo wa wananchi na maeneo hayo.

Sheria hiyo imeelekeza kila taasisi nunuzi Serikali itenge asilimia 30 ya bajeti kwa ajili ya kuyawezesha makundi hayo kushiriki katika zabuni za serikali na hivyo Serikali kupitia PPRA inaanza kutoa mafunzo kuwajengea uwezo juu ya mfumo mpya wa ununuzi ya umma kwa mfumo wa kielektoniki, kanuni wa sheria za manunuzi.

0 Comments