Ticker

6/recent/ticker-posts

BALOZI NCHIMBI AKOSHWA UTEKELEZAJI ILANI KIGOMA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Kigoma na Kamati ya Siasa mkoani humo, kwa utekelezaji wa viwango vizuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, ambapo ndani ya miaka 3 iliyopita takriban shilingi 1.4 trilioni zimepelekwa na kugusa nyanja zote za maendeleo kwa ajili ya wananchi.

Katibu Mkuu Balozi Nchimbi amesema hayo alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa ndani uliofanyika Ukumbi wa Anglikana, Kigoma mjini, leo Jumapili, 4 Agosti 2024.

Post a Comment

0 Comments