Na Adery Masta.
Kampuni namba moja nchini kwa utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo Tanzania , kama ilivyo miaka yote imeendelea kushiriki , Maadhimisho na Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) yanayofanyika Kitaifa jijini Dodoma , Katika Maonesho hayo Kampuni ya Tigo inaendelea na Kampeni yake ya SAKO KWA BAKO yenye lengo la kurudisha kwa wateja wao ambao wameuchagua mtandao wa Tigo , ambapo kupitia Kampeni hii wateja wanapata zawadi mbalimbali wanaponunua vifurushi vya Tigo.
Aidha , Katika maonesho haya Kampuni ya Tigo wamekuja na Simu ya Bei nafuu ya ZTE , akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kati Said Iddi amesema
" Kampuni ya Tigo imewaletea wananchi na wadau wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi simu hii ya ZTE ambayo inatolewa kwa Mkopo na kianzio kikiwa na Tsh. 35000 ( Elfu Thelethini na Tano ) na baada ya hapo mteja atalipa 650 tu kwa siku , Lengo la kuleta simu hii tunataka kuwawezesha wananchi , wakulima na Wavuvi kuweza kupata taarifa sahihi za shughuli zao kwa maana tukimpa simu janja kwa bei nafuu anakua na uwezo wa kutembelea mitandao mbalimbali na kutafuta anachokitaka kwa wakati hasa kupitia mtandao wetu wenye kasi zaidi "
Kwa taarifa zaidi tembelea Banda lolote la Tigo lililopo katika Maonesho ya Nane Nane katika Kanda zote tajwa hapo juu.
0 Comments