Ticker

6/recent/ticker-posts

MGODI WA BARRICK NORTH MARA WASHINDA TUZO KUBWA ZA MWAJIRI BORA 2024


Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi mgodi wa North Mara,Michael Kahela akipokea tuzo ya Mwajiri bora.
Naibu Waziri Mkuu Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akitoa pongezi kwa Meneja Uhusiano wa Barrick, Georgia Mutagahywa kwa ushindi wa North Mara baada ya kumkabidhi cheti.
Wafanyakazi wa Barrick wakisherehekea tuzo 6 za ushindi

**

Mgodi wa North North Mara uliopo wilayani Tarime mkoani Mara ambao unamilikiwa kwa ubia na kampuni ya Barrick na serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga minerals kwa mara nyingine baada ya ushindi wa mwaka jana umeshinda tena tuzo kubwa ya jumla ya mwajiri bora inayotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

Tuzo nyingine ambazo mgodi huo umeshinda ni Uwajibikaji kwa Jamii, Afya na Usalama Mahali pa kazi, Mshindi wa pili katika kipengele cha Mwajiri Bora sekta binafsi, na uzingatiaji wa kanuni za Maudhui ya ndani. Mgodi wa Barrick Bulyanhulu nao umeshinda katika kipengele cha uzingatiaji wa sheria na kanuni kutoka Mamlaka za usimamizi.

Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Mkuu Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.

Akiongelea mafanikio haya ya mgodi wa North Mara, Meneja Uhusiano wa Barrick, Georgia Mutagahywa, alisema ushindi wa tuzo hizi unadhihirisha mgodi huo unavyoendeshwa kwa weredi na viwango vya kimataifa ukitoa kipaumbele kikubwa katika suala la uzingatiaji afya na usalama sambamba na ukuzaji wa vipaji vya Watanzania, Migodi yote ya Barrick inaongozwa na Watanzania na asilimia 96% ya wafanyakazi ni wazawa. Pia kampuni Imekuwa na mpango wa kuwezesha wafanyakazi Wanawake ambapo kwa sasa wanafanya kazi kwa ufanisi katika vitengo mbalimbali.


"Suala la kudumisha uhusiano mzuri na Wafanyakazi linapewa umuhimu mkubwa sambamba na kuendesha programu za kuwajengea afya nje kwa kushiriki mazoezi na michezo mbalimbali",amesema.

Migodi ya Barrick na Twiga pia imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za Serikali kutekeleza miradi ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii za maeneo yanayozunguka migodi yake hususani katika sekta za elimu, Afya, Maji safi na salama na ujenzi wa miundombinu ya barabara.Kati ya mwaka 2020 hadi 2024 Barrick North Mara imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 22 katika kutekeleza miradi 253 ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments