Na Mwandishi Wetu.
Dar es Salaam, Tanzania - Aprili 9, 2025-Benki ya Biashara Tanzania (TCB) kwa kushirikiana na Ramani.io wamezindua rasmi ushirikiano unaolenga kuimarisha biashara za ndani na kuongeza ujumuishaji wa kifedha nchini. Ushirikiano huu unaotarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya biashara, unalenga kuwawezesha wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), wajasiriamali, pamoja na biashara ndogondogo.
Uzinduzi rasmi wa ushirikiano huu umefanyika leo jijini Dar es Salaam na umehudhuriwa na viongozi waandamizi kutoka taasisi zote mbili, wadau muhimu, pamoja na wawakilishi kutoka vyombo vya habari. Tukio hilo pia litashuhudia utiwaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) inayoweka msingi wa ushirikiano huu wa kimkakati.
Kupitia ushirikiano huu, changamoto katika mnyororo wa ugavi na usambazaji zitashughulikiwa kwa kutumia teknolojia bunifu ya Ramani.io sambamba na huduma bora za kifedha kutoka TCB yenye mtandao mpana nchini. Lengo ni kuwawezesha wafanyabiashara kupata mitaji kwa urahisi, kuongeza ufanisi wa uendeshaji, na kukuza biashara zao kwa njia endelevu.
Benki ya Biashara Tanzania inathibitisha tena dhamira yake ya kuwawezesha wafanyabiashara kupitia suluhisho maalum za kifedha kama vile mikopo nafuu, mitaji ya uendeshaji, na elimu ya fedha. Ushirikiano huu unalenga hasa kuwaendeleza wajasiriamali na SMEs ambao ni nguzo muhimu ya ukuaji wa uchumi nchini.
Ushirikiano huu kati ya TCB na Ramani io unaweka kiwango kipya cha ubunifu na ushirikiano katika sekta ya kifedha, ukiwa mfano wa kuigwa wa namna ya kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha na kukuza biashara za ndani. Ni uthibitisho wa wazi wa dhamira ya pamoja ya kuendeleza uchumi jumuishi na endelevu nchini Tanzania.
"Katika Benki ya Biashara Tanzania tunaamini katika kujenga ushirikiano wa maana unaoleta matokeo halisi," Bw.Jesse Jackson, Afisa Mkuu wa Digitali na Ubunifu "Ushirikiano huu na Ramani.io utatusaidia kuwafikia wafanyabiashara wengi Zaidi kwa urahisi na haraka na pia kuwasaidia kukua kwa pamoja na kwa uimara."
0 Comments